Tuzo za Academy Awards maarufu Oscars zitafanyika Machi 2022, mataifa kadhaa barani Afrika tayari yamewasilisha filamu zao ili kushindania tuzo ya Best International Feature Film.
Kenya imewasilisha sinema yake ya kwanza ya kijeshi kwenye Tuzo za Academy Awards maarufu Oscars kwa mwaka wa 2022.
Tume ya Filamu ya Kenya (KFC) imewasilisha filamu ya “Mission to Resue” kwenye awamu ya 94 ya tuzo za Academy Awards kwa mwaka wa 2022.
Filamu “Mission to Rescue” iliyoelekezwa na Gilbert Lukalia na Carna Wambui ilichaguliwa na kamati ya Uchaguzi wa filamu ya Oscars Kenya (OSCK). Filamu hiyo itakuwa inawania tuzo ya Oscars katika kitengo cha Best International Feature Film.
Kenya imewasilisha filamu nyingine awali kama vile “Nairobi Half Life” mwaka wa 2012 katika awamu ya 85 ya tuzo za Oscars. Filamu nyingine zilizowasilishwa ni “Watu Wote” na “The Letter”.
Tuzo za Oscars awamu ya 94 zitafanyika Machi 2022 nchini Amerika. Kufikia Januari 2022, wakenya watajua iwapo filamu ya “Mission to Rescue” itakuwa imeteuliwa kuwania tuzo ya Oscar katika kitengo hicho cha Best International Feature Film na kushindana na filamu zingine kutoka mataifa mengine duniani.
Filamu nyingine kutoka Afrika ambazo zimewasilishwa kuwania tuzo ya Best International Film ni filamu kutoka Malawi iitwayo “Fatsani: A Tale of Survival”, kutoka Morocco “Casablanca Beats”, kutoka Somalia “The Gravedigger’s Wife”, na kutoka Tunisia “Golden Butterfly”.
Zipo filamu nyingi kutoka bara Afrika ambazo zimeshinda tuzo katika kitengo cha Best International Feature Film.
Mfano filamu ya Afrika Kusini “Tsotsi” ilishinda mwaka wa 2005, Ivory Coast ilishinda tuzo ya Oscar mwaka wa 1976 kwa filamu yao ya “Black and White in Colour”. Kutoka Algeria filamu za “Days of Glory” na “Outside the Law” zilishinda tuzo za Oscar mwaka wa 2006 na 2010 mtawalia.
Ili filamu izingatiwe kwa kitengo cha Best International Feature film zi lazima iwe ya zaidi ya dakika 40.