Kikao Kamati Kuu Chadema yazua gumzo

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeanza kikako cha kamati kuu cha chama hicho leo tarehe 08 August,2024 katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama Mikocheni, Jijini Dar es Salaam.

Kikao cha kamati kuu ya Chadema

Hata hivyo kumekuwa na  taarifa huenda  baadhi ya wabunge wa viti maalumu kati ya 19 waliovuliwa uanachama wa Chadema kurejea ndani ya chama hicho.

Kwa mujibu wa viombo vya Habari nchini Tanzania, taarifa Hizo ambazo pia zinazua mjadala wa pande mbili, liliwekwa wazi Agosti 6, 2024 kupitia kauli ya Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalimu kuwa “CCM itamuota sana Mdee juu ya kuhamia katika chama hicho.”

Mkakati huo unaowahusisha baadhi ya viongozi wa Chadema na wabunge wachache wa kundi hilo, umekuwa unakwenda kichinichini na sasa umeshika kasi kipindi hiki ambacho Tanzania inakaribia kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji baadaye mwaka huu na Uchaguzi Mkuu 2025.

Kikao cha kamati kuu ya Chadema

Wabunge hao 19 ni wale ambao Novemba 27, 2020 Kamati Kuu ya Chadema iliwavua uanachama kutokana na uamuzi wao wa kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalumu ilhali msimamo wa chama hicho ulikuwa ni kususia matokeo yote ya uchaguzi mkuu na matokeo yake, zikiwemo nafasi hizo.

Wakati chama hicho hakijakaa kuwateua wabunge hao, kundi hilo liliibuka bungeni na kuapishwa na kuwa wabunge.

Wabunge hao ni Halima Mdee, Ester Bulaya, Esther Matiko, Sophia Mwakagenda, Salome Makamba, Grace Tendega, Cecilia Pareso, Agnes Lambart, Nusrat Hanje, Jesca Kishoa na Hawa Mwaifunga.

Wengine ni Tunza Malapo, Asia Mohammed, Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Kunti Majala, Stella Fiao, Anatropia Theonest na Conchesta Rwamulaza.