Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the wordpress-seo domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/mwanzotv/public_html/wp-includes/functions.php on line 6114
Kimbunga Emnati kimesababisha vifo vya watu wanne nchini Madagascar - Mwanzo TV

Kimbunga Emnati kimesababisha vifo vya watu wanne nchini Madagascar

Takriban watu wanne wamefariki na makumi ya maelfu kuathiriwa baada ya Kimbunga Emnati kushambulia kisiwa cha Madagascar, maafisa walisema Ijumaa.

Madagascar bado inayumba kutokana na kimbunga kingine kilichogonga kisiwa hicho mapema mwezi huu, Emnati iliikumba Madagascar mwanzoni mwa juma, ikibeba upepo wa hadi kilomita 140 kwa saa.

“Kumekuwa na vifo vinne huko Farafangana” mji wa pwani kusini mashariki, kulingana na idadi ya awali ya Ofisi ya Kitaifa ya Kudhibiti Hatari ya Madagascar.

Takriban watu 72,200 wameathiriwa na kimbunga hicho, ambacho pia kilisababisha kukatika kwa barabara na daraja.

Moja ya nchi maskini zaidi duniani, Madagascar inakabiliwa na dhoruba nyingi na vimbunga kati ya Novemba na Aprili kila mwaka.

Dhoruba nyingine, Kimbunga Batsirai, kilipiga kisiwa hicho mnamo Februari 5, na kuathiri watu wapatao 270,000 na wengine 121 kufariki.

Dhoruba ya Tropiki Ana pia ilipiga mwishoni mwa Januari, na kuua takriban watu 100 huko Madagascar, Msumbiji, Malawi na Zimbabwe.

Eneo la kusini mwa Madagascar pia limekumbwa na ukame, na kusababisha utapiamlo kati ya wakazi.