Uapisho wa rais mteule William Ruto utafanyika kesho jumanne tarehe 13 Septemba mwaka 2022 katika uwanja wa kimataifa wa Moi sports centre, Kasarani baada ya mahakama ya upeo kuidhinisha ushindi wake. Mahakama ilitupilia mbali kesi iliyowasilishwa na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga ilikuwa inapinga kuchaguliwa kwa rais mteule William Ruto katika uchaguzi mkuu wa agosti.Uapisho huo utafanywa kuambatana na sheria na naibu rais mteule Rigathi Gachagua pia akitarajiwa kuapishwa siku hiyo.
Masuala ambayo unafaa kujua kuhusu uapisho huo.
Kuchuakua hatamu za uangozi kama rais Kulingana na katiba,
-Uapisho wa rais mteule utafanyika kwa ummma na jaji mkuu na iwapo jaji mkuu hatakuwepo naibu jaji mkuu ataongoza hafla hiyo.
Rais mteule ataapishwa jumanne ya kwanza kufuatia
-Siku 14 baada ya tarehe ya kutangazwa matokeo ya urais, iwapo hakuna kesi imewasilishwa kuambatana na kipengee cha 140 cha katiba.
-Siku ya saba baada ya tarehe ambayo mahakama imetoa uamuzi wake kuidhinisha uchaguzi ikiwa kuliwasilishwa kesi kupinga uchaguzi huo.
- Rais mteule atachukua afisi ya rais kwa kuapa na kuhaidi kuitumikia katiba ya Kenya na kuheshimu afisi ya rais wa taifa ambaye ndiye amiri mkuu wa majeshi.
(2) Nini kitakachotendeka wakati wa uapisho?
–Kuapishwa na kutia saini cheti cha uapisho
-Rais mteule wakati wa hafla ya uapisho, ataapa na kuhaidi kuwa mwaminifu katika kutekeleza majukumu ya afisi ya rais kulingana na kipengee cha 141 cha katiba.
-Kiapo hicho na ahadi kuambatana na ibara ya (1) itatekelezwa kwa rais mteule na kusimamiwa na msajili mkuu wa mahakama ya upeo, jaji mkuu akishuhudia na iwapo jaji mkuu hayupo naibu wake atakuwepo, shughuli hiyo haifai kufanyika kabla ya saa nne asubuhi na pia inafaa kufanyika kabla ya saa nane kamili.
–Baada ya kuapishwa kulingana na kipengee cha (1) cha katiba, rais atatia saini cheti cha uapisho jaji mkuu akiwemo na iwapo hayupo basi naibu jaji mkuu atashuhudia.
–Kukabidhiwa vyombo vya mamlaka na mamlaka
–Baada ya kutia sainicheki cha uapisho, rais anayeondoka atamkabidhi atamkabidhi vyomba vya kazi na mamlaka kwa rais anayeingia. Vyombo hizo ni zifuatazo.
(a) Upanga
(b)Katiba
(2) Hata hivyo shughuli hii haitatekelezwa pale ambapo rais amechaguliwa tena afisini
c) Uapisho wa naibu wa rais mteule
Naibu wa rais mteule ataapishwa na kuhaidi kuwa mwaminifu kwa katiba ya kenya na kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa kipengee cha 148 ya katiba.
d) Hotuba ya uapisho
Rais baada ya kuapishwa kwa naibu wake, atatoa hotuba ya kuapishwa kwa taifa.