Search
Close this search box.
Africa
Roch Marc Christian Kabore, Rais wa zamani wa Burkina Faso

Kiongozi wa chama tawala cha zamani nchini Burkina Faso alikamatwa siku ya Jumapili baada ya kukosoa hali ambayo rais wa zamani Roch Marc Christian Kabore amewekwa na serikali tawala, mawakili wake walisema.

Polisi walimkamata Alassane Bala Sakande nyumbani kwake mapema Jumapili asubuhi na kumleta katika kituo cha polisi cha Paspanga karibu na katikati mwa mji mkuu Ouagadougou, mawakili Antoinette Ouedraogo na Dieudonne Willy walisema katika taarifa.

Katika hafla hiyo Sakande alitoa wito wa kuachiliwa mara moja kwa rais huyo wa zamani ambaye aliondolewa madarakani na mapinduzi ya kijeshi mwezi Januari na amezuiliwa chini ya kizuizi cha nyumbani.

“Kwetu sisi hiki si kifungo cha nyumbani… Anaruhusiwa saa moja kuwaona watoto wake, hawezi kupiga simu, Rais Kabore yuko kizuizini,” Sakande alisema.

Kulingana na wakili wa Sakande mteja wao, ambaye alikuwa rais wa Bunge kabla ya mapinduzi, alihojiwa mbele yao siku ya Jumapili lakini bado alikuwa anashikiliwa na polisi jioni.

Kabla ya kuondolewa madarakani, Kabore alikabiliwa na wimbi la hasira kutokana na uasi wa kijihadi ambao umeharibu nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Chini ya kiongozi wa serikali ya kijeshi Luteni-Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba bunge la mpito lilichukua ofisi huko Ouagadougouo siku ya Jumanne.

Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), zote zimetaka Kabore aachiliwe huru.

Wajumbe wa Afrika Magharibi walimtembelea Kabore wiki jana na kuripoti kuwa alikuwa salama.

Comments are closed