Kiongozi mkuu wa waasi nchini Chad, Tom Erdimi amerejea mji mkuu wa N’Djamena kujiunga na mazungumzo kuhusu mstakabali wa siasa za nchi hiyo.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 67 amerejea nyumbani baada yake kuzuiliwa gerezani kwa miaka miwili nchini Egypt.
Serikali ya Chad ilitangaza Jumanne wiki iliyopita kuwa alisamehewa na rais wa Egypt Abdel Fattah al-Sissi na kuwa atakuwa anarejea Nchini Chad.
Kuwasili kwake kukiwa afueni kubwa kwa ndugu jamaa na marafiki.
Madungu hawa wawili walikuwa wapwa wa aliyekuwa rais wa Chad marehemu Idriss Deby Itno na walikuwa washirika wakuu katika utawala wake miaka ya 1990 kabala ya kuasi serikali yake na kubuni kikosi cha Union of Resistance Forces (URF).
Erdimi amewashukuru wote waliosimama naye katika kile alichokitaja kama ukombozi, akiwemo Kiongozi wa serikali ya mpito Jenerali Mahamat Idriss Deby.
“Kwanza kabisa ningependa kuwashukuru wote…mandugu, wazalendo na wenzangu wote ambao walikusanya raslimali kote duniani kupitia mitandao ya kijamii, kwa kufanya maandamano, kwa kuzungumzo, kupitia njia zote na kwa wote ambao kwa njia moja au nyingine walichangia kufankisha ukombozi huu.” Alisema kiongozi huyo.
Deby alichukua uongozi wa taifa hilo baada ya babake kuuwawa wakati wa operesheni dhidi ya waasi mwaka wa 2021.
Alivunja bunge, akasitisha katiba na kuhaidi kuandaa uchaguzi wa huru na haki baada ya miezi 18 ya utawala wake.
Uchaguzi huo sasa ukitegemea matokeo ya mazungumzo ambayo yalianzishwa na Deby ili kuidhinisha marekebisho ya katiba. Mazungumzo hayo yalianza agosti ishirini na yatadumu hadi septemba thelathini.
Lakini hakujakuwepo na taarifa kamili kuhusu kuwachiliwa kwa kiongozi huyo, ambayo ilikuwa sharti kuu la EFR katika kuhudhuria mazungumzo ya kurejesha uongozi wa taifa hilo kutoka kwa jeshi hadi kwa raia.
Kiongozi huyo ametoa wito wa amani na maridhiano katika kukuza demokrasia nchini humo.
“Bila amani, bila demokrasia, bila utangamano wa nyoyo na fikra hakutakuwa na maendeleo nchini Chad,” alisema kiongozi huyo mara tu baada ya kuwasili.
Aidha Erdimi ametambua mchango wa wahisani wake kutoka mataifa ya kigeni kuhakikisha kwamba anaachiliwa huru na kurejea nyumbani salama salmini.
“Usaidizi wa maana sana wa Sultan wa Qatar Tamim Hamad, ambaye alisaidia mamlaka ya Chad na ambaye pia alishinikiza taifa ambalo lilikuwa limenikamata. Kwa hivyo ningependa kumshukuru mndogo wangu Sultan kwa moyo wangu wote.” Aliongeza Erdimi
Miongoni mwa wafuasi ujio wake umeleta furaha isiyo na kifani, ila kisichofahamika kwa ni jinsi utangamano huo utapiga jeki juhudi za kurejesha amani katika taifa ambalo limekuwa na migogoro kwa miaka na mikaka.