Search
Close this search box.
Kenya

Kitengo cha Mafunzo ya Jeshi la Uingereza nchini Kenya chakumbatia teknolojia mpya ya mafunzo

24
Wanajeshi wa Kenyan.

Kitengo cha Mafunzo ya Jeshi la Uingereza nchini Kenya (Batuk) kimeanzisha teknolojia mpya ili kukabiliana na hofu yoyote ya jamii kuhusu uharibifu wa mazingira wakati wa mafunzo yao.

Batuk vilevile imeanzisha mafunzo ya muigo ya kukabiliana na hali ya mapigano, ambapo wamewafunza wahandisi wa Kenya kuhusu teknolojia hiyo.

“Vifaa vya muigo wa mafunzo vinaendeshwa kwa kawi ya nishati ya jua na vihisi ambavyo vinatoa mtazamo halisi kwa askari na kuongeza nafasi za kuishi kwa wanjeshi katika maeneo ya vita,” amesema Mhandisi Phanice Ayieko Teeka.

Mhandisi Ayieko ni mmoja wa wanafunzi tisa, wanne kati yao wakiwa wanawake, ambao wamejifunza jinsi ya kuutumia vifaa vya mafunzo ya mwigo kujiandaa kwa makabiliano.

“Miigo inajumuisha kazi za kila siku za jeshi ikiwa ni pamoja na mlipuko, mashambulizi yaliyoratibiwa na upigaji raisasi wa usahihi, ambao hupimwa kurekodiwa na kukaguliwa kila siku ili kuboresha utendaji wao,” amesema Teeka.

Amefafanua kuwa teknolijia hiyo itasaidia asakari kurekebisha makosa yao wakati wa mafunzo, na kuongeza kuwa inaboresha nafasi yao ya kujifunza kwa kutoa nakala juu ya oparesheni zao.

 “Kila mwigo unaofanywa na wanajeshi hupitishwa wakati wa mafunzo kwa waendeshaji wanaowafuatilia katika vituo vya tarakilishi vilivyo nje ya mtandao,” alieleza.

Miigo hiyo pia inawatayarisha wanajeshi kwa kile kinachoweza kutokea kwa kutoa changamoto za wakati halisi.

“Kupitia teknolojia, tumesaidia jeshi kuboresha mbinu za kuishi wakati wa hali halisi ya vita,” alisisitiza.

Zaidi ya wanajeshi 5,000 kutoka Uingereza na jeshi la Ulinzi la Kenya wanafanya mazoezi katika eneo la uhifadhi lenye ekari 250,000 huko Laikipia kila mwaka.

Kulingana na afisa wa mawasiliano wa Batuk Meja Adrian Weale, wanajeshi wamekuwa wakitoa tahadharai ili kulinda mazingira na rasilimali za jamii katika  hifadhi dhidi ya uharibifu.

Meja Weale amesema chemikali ambayo kitengo hicho hutumia kwa milipuko ya kijeshi haina madhara kwa mazingira, na kwamba tahadhari za ziada zimechukuliwa kuzuia milipuko ya moto.

Hii inajiri baada ya kisa cha Machi 2021, ambapo zaidi ya ekari 10,000 katika hifadhi ya Lolldaiga ziliharibiwa moto ulipozuka wanajeshi walipokuwa wakifanya mazoezi katika eneo hilo.

Comments are closed

Related Posts