Kocha Mkuu wa Uingereza Gareth Southgate ajiuzulu

Kocha wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate amejiuzulu siku mbili baada ya kushindwa na Hispania kwenye fainali ya Euro 2024. England ilifungwa 2-1 mjini Berlin Jumapili, kikiwa ni kipigo chao cha pili mfululizo katika fainali ya Euro, baada ya kuchapwa kwa penalti na Italia kwenye Uwanja wa Wembley miaka mitatu iliyopita.

 

Kocha huyo mwenye miaka 53 aliiongoza nchi yake kwenye michezo 102 ndani ya miaka minane ya uongozi.

 

Mkataba wake ulikuwa unamalizika baadaye mwaka huu. “Kama Muingereza wa kujivunia, imekuwa heshima katika maisha yangu kuichezea Uingereza na kuinoa England,” alisema Southgate.

 

Mtendaji mkuu wa Chama cha Soka Mark Bullingham amesema mchakato wa kumteua mrithi wa Southgate umeanza na “tunalenga kuwa meneja wetu mpya athibitishwe haraka iwezekanavyo”.

Aliongeza FA “kuwa na suluhu la muda iwapo litahitajika” na hatatoa maoni zaidi kuhusu mchakato huo hadi bosi mpya atakapoteuliwa.

Mechi inayofuata ya England ni dhidi ya Jamhuri ya Ireland katika Ligi ya Mataifa ya Ulaya mnamo Septemba 7.