Rais Uhuru Kenyatta yuko Kisumu kwa ufunguzi rasmi wa kongamano la Toleo la 9 la Africities mjini Kisumu.
Hafla hiyo inafanyika katika Uwanja wa Kimataifa wa michezo wa Jomo Kenyatta.
Miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu waliofika katika mkutano huo ni pamoja na Rais wa zamani wa Jamhuri ya Ushelisheli Danny Faure na Rais wa Umoja wa miji na serikali za mitaa (UCLG) Afrika.
Wengine ni ujumbe wa magavana kutoka Misri ambao ni pamoja na; Dkt Manal Awad wa Damietta, Abdelhamid Elhaggan wa Al Qalyoubia na Balozi Mohamed Higazy.
Viongozi wa eneo hilo akiwemo Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa, Waziri wa Mazingira Keriako Tobiko, Waziri wa Elimu George Magoha na wabunge wengine kutoka eneo hilo.
Balozi wa Africities Lupita Nyong’o, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohamed na Mjumbe Maalum wa Rais wa Marekani kuhusu Hali ya Hewa John Kerry watahutubia wajumbe kupitia mtandao.
Mwenyekiti wa Tume ya Muungano wa Afrika Moussa Faki pia atahutubia kongamano hilo.
Kilele cha hafla hiyo itakuwa hotuba ya Rais Uhuru na kufunguliwa rasmi kwa kongamano hilo.
Zaidi ya watu 200 alijiandikisha kuonyesha bidhaa zao katika mkutano huo.
Kongamano linatarajiwa kuvutia zaidi ya wajumbe 8,000.
Kaulimbiu ya mkutano huo mwaka huu ni, “Wajibu wa miji ya barani Afrika katika utekelezaji wa Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya 2030 na Ajenda ya 2063 ya Umoja wa Afrika.