Kuwait itapiga marufuku filamu ya Agatha Christie whodunnit âDeath on the Nileâ iliyowashirikisha wasanii nyota wa Hollywood akiwemo mwigizaji wa Israel Gal Gadot, mamlaka ilisema Jumapili.
Filamu hiyo iliyooelekezwa na mwigizaji mwenzake Kenneth Branagh, inatarajiwa kutolewa mwezi huu nchini Amerika.
Hadithi hiyo ni moja ya kazi maarufu za mwandishi wa Uingereza Christie, anayeitwa âMalkia wa tamthilia za Uhalifuâ.
Lakini wapenda filamu nchini Kuwait hawataweza kuitazama, msemaji wa wizara ya habari Anouar Mourad aliiambia AFP, akithibitisha ripoti za vyombo vya habari.
Kwa mujibu wa gazeti la Al-Qabas la Kuwait, uamuzi huo umechukuliwa kufuatia matakwa kwenye mitandao ya kijamii kutaka filamu hiyo kupigwa marufuku.
Watumiaji wa mitandao ya kijamii walihoji jinsi Gadot alivyolisifu jeshi la Israel na kukosoa vuguvugu la Kiislamu la Palestina Hamas wakati wa vita vya 2014 huko Gaza.
Vita hivyo vilisababisha vifo vya wapalestina 2,251 wengi wao wakiwa raia na waisraeli 74 wengi wao wakiwa wanajeshi.
Gadot anafahamika zaidi kwa uigizaji nguli wa filamu  za âWonder Womanâ filamu iliyopigwa marufuku katika baadhi ya nchi za kiarabu.
Gadot amekuwa akikosolewa mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu alifanya kazi katika jeshi la Israeli.
Kuwait inapinga vikali kurudisha uhusiano wa kawaida na Israel — tofauti na majirani zake wa Ghuba Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain, ambazo zimetia saini mikataba ya amani na taifa la Kiyahudi — na kwa muda mrefu imekuwa ikunga mkono kadhia ya Palestina.