Libya: Waliokufa Kwa Mafuriko wafikia 11,300

Vikosi vya dharura vinaendelea na zoezi la kuwatafuta maelfu ya watu ambao bado hawajapatikana kutokana na mafuriko makubwa yaliyoukumba mji wa bandari wa Derna mashariki mwa Libya.

Tayari Shirka Shirika la Hilali Nyekundu (Red Crescent) la Libya limesema watu waliokufa imeongezeka na kufikia11,300.

Kulingana na Mkuu wa shirika Hilali Nyekundu, Bi Marie el-Drese, kwamba watu zaidi 10,000 hawajulikani walipo katika mji huo wa pwani wa  Libya.

Hadi kufikia sasa Mamlaka za afya Libya limedhibitisha vifo vya watu zaidi ya 5,500.

Wakati huo huo waziri wa afya wa serikali ya Mashariki ya Libya Othman Abduljaleel amesema wameanza zoezi la kuzika miili ya watu iliyopatikana katika mji wa Derna. Ameongeza kuwa miili mingi imezikwa kwenye makaburi ya pamoja nje ya mjio huo wakati mingine ikipelekwa katika miji na majiji ya karibu.

Kimbunga kikali kilochopewa jina la Daniel kilipiga Libya siku ya Jumapili baada ya kusababisha mabwawa mawili kuvunja kingo zao.