
Miongoni mwa walioshtakiwa ni maafisa watatu wa polisi, Afisa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Nairobi (OCS) aliyesimamishwa kazi Samson Kiprotich Talaam, Konstebo James Mukhwana. Wengine waliotajwa katika kesi hiyo ni John Ngige Gitau, Gin Ammitoa Abwao, na Brian Mwaniki Njue.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), mauaji hayo yalitokea kati ya usiku wa Juni 7 na 8, 2025, ndani ya Kituo cha Polisi cha Nairobi Central, saa chache baada ya Ojwang kukamatwa nyumbani kwao Homa Bay na kuhamishiwa Nairobi. Ripoti ya upasuaji ilionyesha kuwa alifariki kutokana na majeraha ya kichwa, shingo, na michubuko mingi mwilini, ishara ya kushambuliwa kwa ukatili mkubwa.
Haya yanajiri kufuatia uchunguzi wa Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi (IPOA), ambayo iliwasilisha matokeo yake kwa DPP siku moja tu kabla ya kufikishwa mahakamani.
Kifo chake kilizua ghadhabu na maandamano ya umma, na hivyo kuzidisha miito ya kutaka polisi wawajibike.
Albert Ojwang, 31, alipatikana amefariki katika seli ya polisi jijini Nairobi mapema mwezi huu.
Awali polisi walidai kuwa alijitoa uhai hadi madaktari wa serikali walipogundua kuwa ameuawa.
Kesi hiyo iliibua maandamano ya kupinga ukatili wa polisi, malalamiko ya muda mrefu katika nchi hiyo ya Afrika mashariki, ambayo yalikabiliwa na mabomu ya machozi na kundi la “wahuni” wa kulipwa wenye jeuri wiki iliyopita.
Awali Ojwang alikamatwa kwa madai ya kumkosoa naibu mkuu wa polisi Eliud Lagat katika machapisho mtandaoni.
Lagat baadaye alitangaza kujiuzulu kwa muda mnamo Juni 16, 2025, ili kutoa nafasi kwa uchunguzi huru kuhusu.
Katika taarifa yake, Lagat alisema kuwa alichukua hatua hiyo kwa “nia njema na kwa kutambua uzito wa ofisi yake.” Aliahidi kushirikiana kikamilifu na mamlaka za uchunguzi na kueleza kuwa majukumu ya ofisi yake yatachukuliwa na naibu wake hadi uchunguzi utakapo kamilika.
Hata hivyo, hatua hiyo haijatosha kwa baadhi ya viongozi na wanaharakati wa haki za binadamu na waandamanaji wametaka ajiuzulu kikamilifu na mashtaka dhidi yake.
Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) ilisema kwenye X kwamba “imeidhinisha mashtaka ya mauaji dhidi ya watu sita”, wakiwemo maafisa watatu na washukiwa wengine watatu, ambao waliwasilishwa katika Mahakama Kuu ya Kibera jijini Nairobi Jumatatu.
Mapema mwezi huu, Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi ilisema watu 18 walifariki wakiwa mikononi mwa polisi katika muda wa miezi minne iliyopita.
Kifo cha Ojwang kinakuja wakati nyeti huku Kenya ikiadhimisha siku ya Jumatano ya maandamano makubwa yaliyoongozwa na Jenerali Z kupinga serikali ya Rais William Ruto mwaka jana.
Siku ya Jumatatu, msemaji wa serikali alisema hakutakuwa na “maandamano” mnamo Juni 25, badala yake akiwataka watu kuadhimisha nyumbani.
Lakini wiki jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Nairobi George Seda aliwaambia waandishi wa habari maafisa wake walikuwa wamejitayarisha kwa maandamano, akiwataka watu kujizuia na “maandamano ya amani”.