Search
Close this search box.
Africa
Lina Medina akiwa na mtoto wake

Je, umewahi kusikia msichana wa umri wa chini ya miaka 10 akijifungua mtoto?

Yupo msichana wa umri wa miaka 5 ambaye katika mwaka wa 1939 alijifungua mtoto wa kiume.

Msichana huyo kwa jina Lina Medina kutoka nchi ya Amerika Kusini ya Peru alivunja rekodi ya kuwa mama mchanga zaidi duniani kujifungua mtoto akiwa na umri wa miaka 5, miezi 7 na siku 21.

Hili lilikuwa tukio la kustaajabisha kwa wazazi wake, watafiti na hata madaktari.

Kulingana na rekodi za hospitali, Lina alipata ujauzito akiwa chini ya umri wa miaka mitano. Kisa kama cha Lina kinafahamika kama ‘precocious puberty’ ikimaanisha kuwa mtoto huanza kubalehe mapema kabla umri wa kawaida wa miaka 8 kwa wasichana na umri wa miaka 9 wa wavulana.

Lina Marcela Medina alizaliwa tarehe 23 Septemba mwaka wa 1933 mjini Ticrapo, Peru, alikuwa na ndugu wengine nane.

Lina alipokuwa na umri wa miaka 5 na miezi 6, wazazi wake waliona kuwa Lina alikuwa na uvimbe tumboni, walimpeleka hospitali wakiwa na hofu kuwa binti yao ni mgonjwa. Daktari Gerardo Lozada alifanya uchunguzi na kugundua kuwa Lina alikuwa na ujauzito wa miezi saba.

Wazazi wake hawakuamini kuwa mtoto wao alikuwa mjamzito katika umri mdogo namna hiyo. Walimtembelea mtaalamu aliyedhibitisha kuwa kweli Lina alikuwa mjamzito.

Lina alijifungua mtoto wa kiume aliyekuwa na uzani wa kilo 2.7 kupitia upasuaji. Mtoto alipewa jina Gerardo Medina.

Lina Median na mtoto wake Gerardo Medina

Lina hakuwahi kuweka wazi nani aliyempachika ujauzito na pengine hata yeye mwenyewe hakujua ni nani au vipi alipachikwa ujauzito. Babake Lina Tiburelo Medina pamoja na binamu yake walizuia jela kwa muda kwa madai ya kumbaka lakini baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha waliachiwa.

Lina Medina ana umri wa miaka 87 sasa na anasemekana kuishi Peru kwa sasa.

Lina Medina

Kisa cha Lina Medina si cha kipekee, kumekuwa na wasichana wengine ambao wamejifungua watoto wakiwa chini ya umri wa miaka 10.

Mnamo Juni 7 mwaka wa 1932, msichana aliyejulikana kwa herufi ya H alijifungua mtoto akiwa na umri wa miaka 6 na miezi 7. H aliishi India na alifungua mtoto aliyekuwa na uzani wa kilo 1.90 kwa njia ya upasuaji. Katika kisa cha H wazazi wake pia walifikiria alikuwa na uvimbe hadi alipofikishwa hospitali na kupatikana na ujauzito, H alikuwa hajapata hedhi alipopata ujauzito.

Kwingine nchini Usovieti, Msichana kwa jina Liza Yelizaveta Pantueva, aliyezaliwa mnamo Agosti 19 1934 alipata ujauzito akiwa na umri wa miaka 5 baada ya babu yake kumbaka. Liza alijifungua siku chache baada ya kufikisha umri wa miaka 6, ila mtoto wake aliaga dunia.

Kuna visa vingine vya wasichana wa umri wa miaka 8 ambao pia walipata ujauzito na kujifungua. Kutoka Nigeria, msichana kwa jina Mum-Zi aliyezaliwa mwaka wa 1884 alijifungua mtoto akiwa na umri wa miaka 8 na miezi 4. Mum-Zi alikuwa ameolewa kama bibi mdogo wa Chifu Akkiri kutoka kisiwa cha Calabar. Mtoto wake Mum-Zi pia alijifungua mtoto akiwa na umri wa miaka 8 na miezi 8 na hivyo Mum-Zi akawa bibi akiwa na umri wa miaka 17 pekee.

Kutoka China msichana kwa jina Hsi aliyezaliwa mnamo Januari 8 1910, alijifungua mtoto wa liume baada ya kupachikwa ujauzito na mvulana aliyekuwa na umri wa miaka 9. Hsi na mvulana huyo walivunja rekodi ya kuwa wazazi wachanga zaidi duniani.

Comments are closed