Maandamano yakiendelea kuchacha nchini Kenya, nchini Afrika Kusini polisi mambo ni kama hayo baada ya waandamanaji kujitokeza katika miji kadha katika taifa hilo.
Hata hivyo polisi imesema inawazuilia watu 87 kote nchini kuhusiana na maandamano ya upinzani ambayo awali ilitajwa haramu.
Mkuu wa polisi polisi Bheki Cele amesema waliyokamatwa wengi wao ni kutoka katika mji wa Gauteng.
“Wengi walipatikana wakitengeneza vilipuzi vya moto, wakifunga barabara na kujaribu kuwazuia watu kwenda kazini. Hawakuandamana kwa amani ,” alisema.
Bw Cele alisema zaidi ya magurudumu 24,000 yalikamatwa na polisi katika miji tofauti.
Ameongeza kusema polisi wanashirikiana na wanajeshi kuimarisha usalama na kurejesha utulivu.
Chama kikuu cha upinzani ambao ni wachache – Economic Freedom Fighters (EFF) kinaongoza kile knachoitwa ‘’kufungwa kwa shughuli za kitaifa’’. Kilianza maandamano Jumapili saa sita usiku.
EFF kinatoa wito wa kujiuzulu kwa Rais Cyril Ramaphosa na kumalizika kwa mzozo wa nishati nchini humo.