Mamia ya watu, ikiwemo wanaharakati walimiminika jijini Nairobi Jumanne kupinga ongezeko la bidhaa muhimu nchini humo.
Kenya imeshuhudia ongezeko la bidhaa muhimu kwa muda sasa, hii ikitokana na janga la UVIKO 19 na hata mashambulizi ya Urusii dhidi ya Ukraine.
Kulingana na utafiti bei ya bidhaa muhimu kama vile unga wa mahindi, mafuta ya kupikia na unga wa ngano imeongezeka kwa 20% mnamo Januari 2022 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mnamo 2021.
Kufikia mwisho wa Februari 2022, Wakenya milioni 3.1 kati ya milioni 47 walikuwa wanahitaji msaada wa chakula.
Mfumuko wa bei ya vyakula kwa mwezi wa Januari ulisimama kwa 9%, kumaanisha Wakenya wengi walitatizika kuweka chakula mezani.
Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya (KNBS) inasema kwa kaya maskini, ambapo chakula kinachukua takriban 36% ya jumla ya matumizi, mzigo ni mkubwa zaidi.
Kuongezeka kwa gharama ya maisha kunaweza kuhusishwa na mchanganyiko wa mambo ya nje na ya ndani.
Chini ya shinikizo kutoka kwa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kuongeza mapato zaidi, serikali imeongeza ushuru kwa bidhaa za kila siku za nyumbani kama vile gesi ya kupikia na mafuta ya kupikia.
Kundi la Njaa Revolution, katika maandamano yao leo linapinaga kufanyika kwa uchaguzi Agosti 9 iwapo bei ya bidhaa muhimu haitapunguzwa
Ongezeko la Bei
Bidhaa Bei ya awali Bei Mpya
Mkate ksh50 ksh 60
Sukari 1kg Ksh 114 Ksh 150
2kgs Unga wa Ugali Ksh 90 Ksh 120
½ lita Maziwa Ksh 50 Ksh 60
Mafuta ya kupikia1 lita Ksh 220 Ksh 300
Benki ya Dunia ilikuwa imekadiria kwamba uchumi wa Kenya utakua kwa 5% mwaka wa 2022. Ila wakenya wanataka kuhisi ukuaji huo kibinafsi.