Search
Close this search box.
Africa

Maandamano ya Millions March kufanyika Jumamosi 30 Oktoba.

14
Maandamano ya Millions March mwaka wa 2019

Mapinduzi ya tano yaliyofaulu yalifanyika Sudan siku ya Jumatatu 25 Oktoba. Mapinduzi hayo yaliongozwa na mkuu wa jeshi jenerali Abdel Fattah al Burhan aliyekuwa katika muungano wa uongozi na Waziri mkuu Abdalla Hamdok katika serikali ya mpito.

Kutoka Jumatatu waandamanaji wamekuwa wakiandamana katika mji mkuu Khartoum kupinga mapinduzi hayo na kudai kurejeshwa kwa uongozi wa kiaria nchini humo.

Kulingana na taarifa takriban watu saba wameuawa kutoka Jumatatu na wengine 21 wamejeruhiwa.

Muungano wa Afrika AU umesitisha Sudan kushiriki katika shughuli za muungano huo kwa muda nayo Benki ya Dunia imezuia ufadhili wa dola milioni 700 wakipinga mapinduzi hayo.

Jenerali Burhan anaendelea kusisitiza kuwa uchaguzi wa kidemokrasia bado utafanyika 2023, ila mapinduzi hayo yalibidi yafanyike ili kuepuka vita vya wenyewe kwa wenyewe, alisema jenerali Burhan.

Waandamanaji ambao wamekuwa wakipinga mapinduzi hayo na kudai kurejeshwa kwa uongozi wa raia wamepanga kufanya maandamano makubwa Jumamosi 30 Oktoba. Maandamano hayo yanajulikana kama Millions March.

Si mara ya kwanza kwa maandamano hayo ya Millions March kufanyika Sudan, yamefanyika tena mwezi Julai mwaka wa 2019 yalipotumiwa kushinikiza kurejeshwa kwa uongozi wa kiraia baada ya kuondolewa madarakani kwa Rais Omar al Bashir.

Katika maandamano ya Millions March ya 2019 watu saba waliuawawa na wengine 181 kujeruhiwa baada ya maelfu ya waandamanaji kumiminika katika barabara za Khartoum na Omdurman kutafuta haki kwa mamia ya wahasiriwa wa ukandamizaji mbaya wa kijeshi.

Rais Omar al Bashir aliondolewa madarakani baada ya maandamano ya miezi kadhaa ya kupinga uongozi wake. Mara tu alipoondoka chama cha Baraza la Mpito la Kijeshi (TMC) kilichochukua uongozi wa taifa kilitofautina na walioongoza maandamano ya kumundoa Omar al Bashir.

Mwaka huo wa 2019 maelfu ya waandamanaji walihamasishwa kushiriki maandamano kupitia mtandao.

Jumamosi 30 OKtoba, maelfu ya waandamanaji wanaodai uongozi wa kiraia watakuwa wanamiminika tena katika barabara za Khartoum, Omdurman na miji mingine katika Millions March kudai kurejeshwa kwa uongozi wa kiraia.

Millions March mwaka wa 2019

Comments are closed

Related Posts