Mtu mmoja amepigwa risasi katika soko la Toi karibu na mtaa duni ya Kibera, Nairobi, wakati maandamano iliyoitishwa na Upizani yakiendelea kunoga maeneo kadhaa ya taifa la kenya.
Hata hivyo inasemekana jamaa aliyepigwa Risasa ni fundi mitambo wala si muandamanaji Kama ilivyodhaniwa.
Kulingana na waliyoshuhudia, jamaa huyo alipigwa risasi na polisi . hata hivyo wakaazri walimkimbiza hospitalini kwa pikipiki mara moja.
Hayo yakiendelea ni kuwa Polisi wa kutuliza ghasia jijini Nairobi wamewarushia mabomu ya kutoa machozi wakaazi wa kitongoji duni kikubwa zaidi katika mji mkuu wa Nairobi, ili kuwazuia kuandamana hadi katikati mwa jiji kwa ajili ya maandamano yaliyopangwa na upinzani.
Polisi wamepinga kambi maeneo kadha jijini Nairobi na Kisumu huku barabara zote za kuelekea kwenye ikulu ya Nairobi ikiwa imefungwa na njia ya kuelekea ikulu ndogo ya Kisumu pia imefungwa.
Makundi na Milolongo mifupi imeshuhudiwa katika mitaa ya Nairobi wakati polisi wanakabiliana na waandamanaji.
Hadi kufikia sasa kiongozi wa azimio Raila Odinga hajajitokeza kwenye maandamano hayo. Inadaiwa kuna baadhi ya viongozi wa upizani waliyozuiliwa kutoka katika makaazi yao.
Wengine kama vile Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Seneti Stewart Madzayo na mwenzake wa bunge Opiyo wandayi wamekamatwa na polisi.
Upinzani umeitisha maandamano makubwa yaliyopangwa kupinga gharama ya juu ya maisha na kile wanachokiita urais usio halali.