Madaktari wasitisha mgomo Kenya

(Picha// SIMON MAINA / AFP)

Mgomo wa muda mrefu wa madaktari hatimaye umefikia kikomo baada ya siku 56 huku serikali na Muungano wa Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno nchini (KMPDU) wakiafikiana.

Haya yanajiri baada ya Mahakama ya Ajira na Mahusiano ya Kazi kuamuru chama cha wafanyakazi na serikali kuja na kanuni inayokubalika ya kurejea kazini kufikia Jumatano.

KMPDU mnamo Jumanne iliwasilisha mbele ya mahakama hati tofauti na ile ambayo serikali ilikuwa imewasilisha, na kumfanya jaji kutoa makataa ya Jumatano, akisema ikiwa italazimika kuamua suala hilo.

Muungano na mashirika ya serikali – kupitia Baraza la Magavana (CoG) na Wizara ya Afya – walikuwa kwa sehemu bora ya Jumanne jioni katika mkutano wa kutatua swala la madakatari

Katibu Mkuu wa KMPDU Dkt. Davji Atellah alikuwa, kwa wakati huo, ameahirisha maandamano ya amani ya madaktari hadi tarehe ambayo haijatajwa ili kuandaa njia ya mazungumzo.

photo coutesy

Tangu Machi 14, madaktari wameacha vituo vyao vya kazi na wamekuwa wakipinga serikali kushindwa kuwapa kazi wanagenzi wa wahudumu wa afya na Mkataba wa Majadiliano ya Pamoja (CBA) wa 2017 kuhusu masharti ya kazi ya madaktari.

Wamefanya mazungumzo ya muda mrefu na kamati ya ‘Njia ya Taifa zima’ inayoleta pamoja Wizara ya Afya, Tume ya Mishahara na Marupurupu na Mkuu wa Utumishi wa Umma.