Taarifa kuhusu Cameroon, Ghana, Morocco, Senegal na Tunisia, mataifa matano ya Afrika yaliyofuzu wiki hii kwa Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar.
Watagundua ni wapinzani gani wa makundi matatu ambao kila timu itakutana nao wakati droo ya mchuano huo wa timu 32 itakapopangwa mjini Doha siku ya Ijumaa.
Hili ni Kombe la Dunia la kwanza kufanyika Mashariki ya Kati na litaanza Novemba 21 na fainali inatarajiwa kufanyika Desemba 18.
Cameroon
Jina maarufu la Cameroon: Indomitable Lions:
Wanashikilia nafasi ya sita 6 barani Afrika: 38 duniani
Nahodha wa timu ni Vincent Aboubakar; Kocha ni Rigobert Song
Waliofunga mabao: 3 – Eric Maxim Choupo-Moting, Karl Toko Ekambi; Vincent Aboubakar, Christian Bassogog, Michael Ngadeu-Ngadjui; Nicolas Ngamaleu, Andre-Frank Zambo Anguissa
Mechi za awali katika Kombe la Dunia: Wameshiriki mara 7 (Miaka ya1982, 1990, 1994, 1998, 2002, 2010, 2014)
Walifika robo fainali (1990)
Ghana
Jina maarufu la timu: Black Stars
Inashikilia nafasi ya 11 barani Afrika, 61 duniani
Nahodha wa timu ni Andre Ayew ; Kocha ni Otto Addo
Waliofunga mabao 3 – Andre Ayew, Thomas Partey;</b> <i>1 – Mohammed Kudus, Mubarak Kudus.
Timu ya Ghana imeshiriki katika mara 3 kwenye Kombe la Dunia (2006, 2010, 2014)
Ghana ilifika robo fainali (2010)
Morocco
Morocco Jina maarufu: Atlas Lions
Wanashikilia nafasi ya 2 Afrika, 24 duniani
Nahodha ni Romain Saiss; Kocha ni Vahid Halilhodzic
Waliofunga mabao 5 – Ayoub el Kaabi; Ryan Mmaee; Selim Amallah, Achraf Hakimi, Imran Louza, Azzedine Ounahi, Tarik Tissoudali, Selim Amallah, Achraf Hakimi, Imran Louza, Azzedine Ounahi, Tarik Tissoudali.
Timu ya Morocco imeshiriki Kombe la Dunia mara 5 katika miaka (1970, 1986, 1994, 1998, 2018)
Senegal
Senegal jina maarufu: Teranga Lions
Inashikilia nafasi: 1 Afrika, 18 duniani
Nahodha ni Kalidou Koulibalay na Kocha ni Aliou Cisse
Waliofunga mabao 4 – Famara Diedhiou, Sadio Mane, Ismaila Sarr, Boulaye Dia, Keita Balde, Abdou Diallo, Habib Diallo, Idrissa Gueye
Walishiriki Kombe la Dunia mara 2 (2002, 2018)
Walioweka nafasi nzuri zaidi katika Kombe la Dunia kwa kufika robo fainali (2002)
Tunisia
Tunisia jina maarufu: Carthage Eagles
Wanashikilia nafasi ya 5 Afrika na 36 duniani
Nahodha wa timu ni Wahbi Khazri na Kocha ni Jalel Kadri
Wafungaji: 3 – Wahbi Khazri; Ellyes Skhiri; Dylan Bronn, Mohamed Drager, Seifeddine Jaziri, Aissa Laidouni, Ali Maaloul, Anis Ben Slimane, Moussa Sissako (MLI)
Walishiriki Kombe la Dunia mara 5 (1978, 1998, 2002, 2006, 2018)