Search
Close this search box.
Africa
Waandamanaji wanaopinga Rwanga nchini DRC wakiendelea na maandamano.

Maelfu ya waandamanaji wanayoipinga Rwanda waliandamana katika mji wa Goma mashariki mwa jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku ya jumatatu, huku waasi wa M23 wakiimarisha udhibiti wao katika maeneo ya mashambani.

Kundi la M23 lililojaa Watutsi, lilianza tena mapigano mwishoni mwa 2021 baada ya kusalia kimya kwa miaka mingi wakiishutumu serikali ya jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa kushindwa kuheshimu makubaliano ya kuwajumuisha wapiganaji wake katika jeshi.

Kuibuka upya kwa kundi hilo kumevuruga uhusiano wa kikanda wa Afrika ya kati, huku Grc ikishutumu jirani yake Rwanda kwa kuwaunga mkono wanamgambo wa M23.

Waasi katika siku za hizi karibuni waliteka miji ya Kiwanja na Rutshuru kando ya barabara kuu inayoelekea mji mkuu wa mkoa wa Goma ambao upo kwenye mpaka wa Rwanda.

Serikali ya DRC iliamua kumfukuza balozi wa Rwanda siku ya jumamosi. Rwanda ilisema kuwa imetambua uamuzi huo kwa masikitiko makubwa.

Balozi, Vincent Karega aliondoka DRC siku ya jumatatu.

Maelfu ya watu waliandamana dhidi ya Rwanda mjini Goma siku hiyo hiyo, ambapo maafisa wa polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya kutoka kituo cha mpaka nan chi hiyo.

“Tunakemea unafiki wa jumuiya ya kimataifa wakati wa uvamizi wa Rwanda” alisema Mambo Kawaya, mwakilishi wa mashirika ya kiraia aliyehudhuria maandamano hayo.

Waandamanaji waliimba na kuomba silaha za kupigana na taifa la Rwanda, pamoja na kauli mbiu za chuki dhidi ya Uganda ambayo baadhi pia wanaituhumu kuwa inaunga mkono M23.

Kundi hilo la waasi lilipata umaarufu kwa mara ya kwanza mwaka wa 2012 wakati lilipoiteka Goma kwa muda mfupi kabla ya mshambulizi ya pamoja kati ya Congo na umoja wa mataifa kuliondoa.

Ni mojawapo ya makundi mengi yenye silaha ambayo yanazunguka mashariki mwa DRC, mengi yakiwa ni urithi wa vita viwili vya kikanda vilivyopamba moto mwishoni mwa karne iliyopita.

Lakini licha ya Kigali kukanusha rasmi, ripoti ambayo haijachapishwa ya umoja wa mataifa iliyoonekana mwezi agosti iliashiria kuhusika kwa Rwanda na M23.

Ripoti hiyo ilisema M23 inapanga kukamata Goma, kitovu muhimu cha biashara cha takriban watu milioni moja, ili kupata makubaliano ya kisiasa kutoka kwa serikali ya Congo.

Rais wa Rwanda Paul Kagame alitumia ujumbe kwenye ukurusa wake wa twita siku ya jumatatu kuwa alikuwa na mazungumzo na mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuhusu jinsi ya kupunguza hali hiyo.

Comments are closed