Mahakama Kuu ya Nakuru imesitisha agizo la Rais William Ruto kubuni jopo la kutathmini deni la kitaifa kenya .
Hakimu Lawrence Mugambi amesitisha utekelezaji wa kubuniwa kwa jopo hilo hadi pale kesi hiyo itakaposikizwa na kuamuliwa.
Rais William Ruto Ijumaa iliyopita alichapisha kwenye gazeti rasmi la serikali kubuniwa kwa jopo kama mojawapo ya mikakati ya kudhibiti hali baada ya kutupilia mbali mswada wa fedha wa mwaka 2024.
Jopo hilo lilijukumiwa kugagua deni la kitaifa katika muda wa siku 90 na kuwasilisha ripoti kwa Rais.
Kulingana na mwasilishi wa kesi hiyo, Rais Ruto alikiuka sheria kuunda jopo hilo ilihali ukaguzi huounapaswa kufanya na mhasibu mkuu wa serikali.
Mahakama hiyo itatoa mwongozo zaidi Julai 23.