Mahakama ya rufaa nchini Kenya siku ya Ijumaa iliondoa kusimamishwa kwa nyongeza ya ushuru iliyozua utata ambayo imesababisha maandamano ya upinzani, kuruhusu serikali kuongeza ushuru hadi uamuzi wa mwisho utakapotolewa.
Rais William Ruto mwezi uliopita alitia saini kuwa sheria mswada wa fedha unaotarajiwa kuzalisha zaidi ya dola bilioni 2.1 kwa hazina ya serikali iliyopungua, lakini ushuru huo unatishia kuongeza shinikizo zaidi kwa watu ambao tayari wanakabiliwa na mfumuko wa bei.
Mahakama kuu ya Nairobi ilikuwa imesitisha utekelezwaji wa sheria hiyo baada ya seneta kuwasilisha kesi kupinga uhalali wake wa kikatiba. Lakini siku ya Ijumaa, mahakama ya rufaa iliondoa zuio hilo, ikisubiri uamuzi wa mwisho kuhusu kesi hiyo.
“Amri inayokataza utekelezwaji wa Sheria ya Fedha ya 2023… inaondolewa hadi inasubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa rufaa,” benchi ya majaji watatu iliamua.
Uamuzi huo unajiri baada ya miezi kadhaa ya maandamano dhidi ya serikali ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwa sehemu kuhusu mgogoro wa gharama ya maisha, huku maandamano hayo yakizidi kuwa uporaji na mapigano makali na polisi.
Machafuko hayo yamezua taharuki miongoni mwa Wakenya na jumuiya ya kimataifa, ambayo imezitaka pande hizo mbili kujadiliana suluhu la kisiasa.
Serikali inasema ushuru huo utasaidia kuunda nafasi za kazi na kupunguza ukopaji wa umma.
Kwa kupuuza maagizo ya awali ya kusimamishwa, mdhibiti wa nishati nchini Kenya mwezi uliopita alitangaza kupanda kwa bei ya pampu baada ya kuongezeka maradufu kwa VAT hadi asilimia 16 kama ilivyoainishwa katika sheria.