Search
Close this search box.
Politics
Naibu rais wa Kenya Rigathi Gachagua.

Mahakama ya kupambana na ufisadi imeruhusu ombi la afisi ya mkurugenzi wa mashataka ya umma kuondoa kesi ya ufisadi ya bilioni 7.5 dhidi ya naibu rais Rigathi Gachagua.

Kesi hiyo imefutwa chini ya kifungu cha 87 kwa kukosa ushahidi.

Hakimu Victor Wakumile alionya na kufahamisha washtakiwa kuwa wanaweza kukamatwa tena katika siku zijazo kwa makosa kama hayo.

Alisema ushahidi uliowasilishwa unapaswa kuthibitisha waziwazi kuwa mshukiwa ana kesi ana kesi ya kujibu.

Katika kuruhusu ombi la Mkurugenzi wa mashataka ya umma, Wakumile alisema mtu hawezi kupendelea mashtaka kwa kutarajia kupata ushahidi.

Hata hivyo amekinyoshea kidole cha lawama asasi za uchunguzi kwa kuwasilisha watu mahakamni wakati bado wanaendelea na uchunguzi kuwahusu.

“Uamuzi wa malipo lazima utekelezwe kwa sehemu na kwa uhuru” alisema hakimu Wakumile.

“Kamwe mfumo wa mahakama haupaswi kutumika kama kwa njia isiyofaa. Kuna hata ya kuheshimu taasisi hapa nchini.”

Mahakama imesema dhamana ya milioni 12 ambayo Gachagua aliweka kortini kama sharti la kuachiliwa kwake aliposhtakiwa inapaswa kurejeshwa kwake.

Pasipoti yake pia itarejeshwa.

Hali hiyo itatumika kwa washtakiwa wengine vilevile.

Hapo awali, afisa wa polisi Kuriah Obadiah aliapa hati kiapo akisema maafisa wa upelelezi katika idara ya Jinai (DCI) walilazimishwa kumshtaki Gachagua katika kesi hiyo ya ufisadi.

Comments are closed