Mahakama kuu ya Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano iliiamuru Uganda kuilipa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo dola milioni 325 kutokana na vita vya kikatili miongo miwili iliyopita, ikiwa ni sehemu ndogo tu ya kile Kinshasa ilidai.
Uamuzi huo wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) unakuja kama pigo kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kutaka fidia kubwa ya dola bilioni 11 kutokana na mzozo huo mbaya uliodumu kutoka 1998 hadi 2003.
Majaji walisema Kinshasa imeshindwa kuthibitisha iwapo Uganda ilihusika moja kwa moja na vifo vya zaidi ya watu 15,000 kati ya mamia ya maelfu ya watu wanaoaminika kufariki katika vita hivyo.
Mahakama imeamua Uganda illipe fidia iliyotolewa kwa DRC, ambayo ni dola za Amerika milioni 325,” alisema Joan Donoghue, hakimu mkuu wa mahakama hiyo yenye makao yake makuu Hague.
Ikifafanua takwimu hiyo, mahakama ilisema Uganda lazima ilipe dola milioni 225 kwa atahri iliyosababishiwa watu, ikiwa ni pamoja na vifo, majeraha na unyanyasaji wa kingono, na dola milioni 40 kwa uharibifu wa mali.
Ni lazima pia kulipa dola milioni 60 kwa uharibifu wa maliasili, ikiwa ni pamoja na uporaji wa coltan, madini ya metali yanayotumika katika simu na kompyuta, na malighafi nyinginezo pamoja na uharibifu wa misitu na uharibifu wa wanyamapori.
Mwaka 2005 ICJ iliamua kwamba Uganda ilipaswa kulipa fidia, lakini nchi hizo mbili hazikuwahi kukubaliana kiasi cha fidia kitakacholopiwa.
Kisha Kinshasa ilidai zaidi ya dola bilioni 11 kwa Uganda kukita kambi katika eneo la kaskazini mashariki la Ituri.
Katika kilele cha mzozo nchi, tisa za Kiafrika zilijunga kwenye mzozo huku Uganda na Rwanda zikiunga mkono vikosi vya waasi dhidi ya serikali ya Kinshasa wakati wakipambana kudhibiti eneo lenye utajiri wa madini la Ituri.
Mahakama ya ICJ Ilianzishwa baada ya Vita Kuu vya Pili vya Dunia, mjini The Hague ikiwa na jukumu la kutatua migogoro kati ya nchi, hasa kwa kuzingatia mikataba iliyopo.
Maamuzi yake ni ya mwisho na hayawezi kukata rufaa.
Hivi sasa wanajeshi wa Congo na Uganda wamerejea katika eneo hilo, lakini safari hii katika mashambulizi ambayo hayajawahi kushuhudiwa dhidi ya Allied Democratic Forces, wanamgambo walioua zaidi katika eneo hilo, ambalo kundi la Islamic State linaita mshirika wake.
Katika shambulio la hivi punde linaloshukiwa la waasi wa ADF, watu watatu waliuawa siku ya Jumamosi katika eneo la Beni katika jimbo jirani la Kivu Kaskazini.