Watu zaidi ya 40 wameripotiwa kufariki dunia kutokana na mapambano mapya kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF mapema wiki hii katika mji wa El-Fasher, Darfur.
Washambulizi ya angani, makombora na milio ya risasi yameripotiwa kurindima mji wa El-Fasher tangu siku ya Ijumaa ya tarehe 10 mwezi huu, hii ni kulingana na walioshuhudia.
Taarifa ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa takriban watu zaidi ya 850 wameachwa bila makao, kutokana na makabiliano hayo yaliyodumu kwa saa nzima.
Kulingana na ripoti kutoka kwa Umoja wa mataifa, Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu pamoja na wahudumu wa afya wameshindwa kutoa taarifa ya kinachoendelea kutoka mji huo, kutokana na njia ya mawasiliano kukatika.