Rais Uhuru Kenyatta amewateua Juliana Cherera, Francis Wanderi,Irene Masit na Justus Nyangaya kuwa makamishna wapya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa muda wa miaka 6 baada ya kuidhinishwa na bunge.
Usaili wa kujaza nafasi nne za makamishna wa IEBC ulianza mapema Julai 2021 na watu 36 waliokuwa wametuma maombi ya kazi. Watu hao 36 walifika mbele ya jopo lililochukua wiki mbili kufanya usaili huo. Makamishana hao 6 wanajaza nafasi zilizoachwa wazi baada ya kuondoka kwa Roselyn Akombe, Margaret Mwachanya, Paul Kurgat na aliyekuwa naibu mwenyekiti Consolata Maina aliyejiuzulu baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.