Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the wordpress-seo domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/mwanzotv/public_html/wp-includes/functions.php on line 6114
Malawi yatangaza mlipuko wa polio - Mwanzo TV

Malawi yatangaza mlipuko wa polio

Kisa cha kwanza cha virusi vya polio barani Afrika katika zaidi ya miaka mitano kimegunduliwa kwa mtoto mdogo nchini Malawi, Shirika la Afya Duniani lilisema Alhamisi.

Mamlaka ya afya ya Malawi imetangaza kuzuka kwa virusi vya polio aina ya 1 baada ya kisa kugunduliwa katika mji mkuu Lilongwe, WHO ilisema.

Uchambuzi wa kimaabara ulionyesha kuwa aina iliyogunduliwa inahusishwa na ile ambayo imekuwa ikizunguka katika Mkoa wa Sindh nchini Pakistani.

Polio ni ugonjwa ambao umeendela kuaathiri watoto nchini Pakistan na Afghanistan.

“Kwa kuwa kisa hiki kimekuja kutoka Pakistani, ugunduzi huu hauathiri hali ya uthibitisho wa virusi vya polio katika kanda ya Afrika,” WHO ilisema.

Afrika ilitangazwa kuwa haina polio mnamo Agosti 2020 baada ya kuondoa aina zote za polio.

Hakuna kesi ya polio iliyokuwa imetokea katika bara hili kwa miaka minne iliyopita.

“Kufuatia kugunduliwa kwa polio aina hii kali nchini Malawi, tunachukua hatua za haraka kuzuia uwezekano wake wa kuenea,” mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Matshidiso Moeti alisema katika taarifa yake.

“Kwasababu ya kuwa kiwango cha juu cha ufuatiliaji wa polio katika bara na uwezo wa kugundua virusi haraka, tunaweza kuzindua harakati za haraka na kuwalinda watoto kutokana na athari mbaya za ugonjwa huu.”

WHO ilisema inaunga mkono Malawi katika kufanya tathmini ya hatari na kukabiliana na mlipuko, ikiwa ni pamoja na chanjo ya ziada.

“Kisa cha mwisho cha virusi vya polio barani Afrika kiligunduliwa kaskazini mwa Nigeria mwaka 2016 na duniani kote kulikuwa na wagonjwa watano tu mwaka 2021. Kesi yoyote ya virusi vya polio ni tukio kubwa na tutakusanya rasilimali zote kusaidia nchi inayoathirika,” alisema Dk. Modjirom Ndoutabe, mratibu wa polio wa WHO kanda ya Afrika.

Poliomyelitis — neno la kimatibabu la polio — ni virusi vya kuambukiza ambavyo hushambulia uti wa mgongo na kusababisha ulemavu usioweza kutenduliwa kwa watoto.

Virusi vya polio kwa kawaida huenezwa kwenye kinyesi cha mtu aliyeambukizwa na huchukuliwa kupitia maji au chakula kilichochafuliwa.

Ingawa hakuna tiba ya polio, kuwachanja watu ili kuwazuia kuambukizwa ndio huvunja mzunguko wa maambukizi.

Tamko la Agosti 2020 kwamba Afrika haikuwa na virusi vinavyosababisha polio lilikuwa alama muhimu katika kampeni ya miongo kadhaa ya kutokomeza ugonjwa huo mbaya kote ulimwenguni.

Ugonjwa huo ulikuwa wa kawaida kote ulimwenguni hadi chanjo ilipopatikana katika miaka ya 1950, ingawa hii ilibakia nje ya kufikiwa na nchi nyingi maskini zaidi za Asia na Afrika hadi msukumo mkubwa katika miongo ya hivi karibuni.

Mwaka 1996, kulikuwa na zaidi ya kesi 70,000 katika Afrika pekee.