Mwanamke mmoja alikamatwa na kisha kusafirishwa katika hospitali ya wagonjwa wa akili siku ya Jumanne baada ya watoto wake wawili wachanga kupatikana wakiwa wamekatwa kichwa katika eneo la ng’ambo la Karibea la Guadeloupe nchini Ufaransa, kulingana na mwendesha mashtaka.
Watoto hao wenye umri wa mwaka mmoja na minne walipatikana nyumbani kwa mama huyo katika kijiji cha Sainte-Rose.
Kulingana na mwendesha mashtaka Caroline Calbo, mwanamke huyo, mwenye umri wa miaka, 40, aligundulika kutokuwa sawa kiakili na kuhamishiwa katika hospitali ya wagonjwa wa akili.
Polisi wameanzisha uchunguzi wa kubaini kilichojiri na kupelekea mauaji hayo ya kinyama kwa Watoto hao wachanga.
Ripoti zinasema kuwa , mume wa mwanamke huyo alipiga simu kwa polisi kabla ya alfajiri baada ya kugundua miili ya watoto hao.
Idhaa ya redio ya eneo hilo RCI Guadeloupe ilisema baba huyo alikuwa na mshtuko.
Hadi sasa vyanzo nchini humo vinasema kuwa mama huyo amekuwa hajielewi na kushindwa kueleza kilichotokea.