Search
Close this search box.
Europe

Mama Akiri Kumuua Mwanawe Mwenye Saratani

427

Mama aliyekuwa na mtoto mwenye saratani amekiri mbele ya mahakama kuhusika katika kumuua mwanawe.

Mama huyo alikiri kumpa mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka saba,  kipimo kikubwa cha “morphine” ili kukomesha mateso aliyosema alikuwa akipitia  na “kumaliza maisha yake kimya kimya”.

Mama huyo kwa jina, Antonia Cooper, kutoka Abingdon, Oxfordshire, alisema mwanawe Hamish alikuwa na saratani ya hatua ya nne na alionekana akiwa katika “maumivu makali” kabla ya kufariki mwaka 1981.

Wakati wa mahojiano na BBC Radio huko Oxford, katika mjadala wa ‘jaribio linalolenga kubadilisha sheria na kuruhusu “kusaidiwa kufariki dunia” kwa watu wanaoteseka’, mama huyo aliweka bayana kuwa kwa sasa anaugua saratani.

Ikumbukwe kuwa kusaidia mtu kufariki dunia, au kumsaidia mtu mwingine kimakusudi kumaliza maisha yake, ambayo pia huitwa “euthanasia” au “kumaliza maisha ya mtu kimakusudi”, ni kinyume cha sheria nchini Uingereza.

Comments are closed

Related Posts