Mamba ashukiwa kumla mtoto nchini Australia

Mtoto mwenye umri wa miaka 12 anahofiwa kuuawa na mamba kaskazini mwa Australia.

Mtoto huyo ambaye alionekana akiogelea karibu na mji wa mbali wa Nganmarriyanga umbali wa takribani saa 7 kwa gari kuelekea kusini magharibi mwa Darwin, anaripotiwa kuonekana mara ya mwisho jioni ya Jumanne.

Ripoti kutoka kwa polisi nchini humo imethibitisha timu ya wataalamu wa utafutaji na uokoaji wametumwa kuendeleza msako mkali wa kumtafuta mtoto huyo, huku maafisa wa ziada na timu ya utaftaji na uokoaji wa kitaalamu ambao wanatafuta nchi kavu na majini, wakiwa wameongezwa.

Ripoti kutoka vyombo vya habari vya ndani, nchini humo vile vile pia vinaweza  kuanza.

Eneo hilo inajulikana sana kwa makadirio ya mamba takriban 100,000 wa maji ya chumvi, idadi hii ikiwa ni zaidi ya pahali popote duniani, ila mashambulizi kama hayo kutukia inaripotiwa kuwa si ya kawaida.