Kutoka eneo la kaskazini mwa Kenya lililokumbwa na ukame, watu wa Purapul wanakaribia kufa na njaa, hawana chochote cha kula ila matunda ya pori huku watoto wao wakiugua utapia mlo.
Loka Metir anajua matunda chungu huwafanya watoto wake kuwa wagonjwa, na hivyo kudhoofisha hali yao hata zaidi.
Lakini mvua haijanyesha ipasavyo kwa miaka mitatu, na hakuna kitu kingine cha kula.
“Hii ndiyo njia pekee ya kuishi,” mama huyo wa watoto watano aliambia shirika la habari la AFP huko Purapul, eneo lililoumbali wa siku mbili kutoka mji wa karibu katika kaunti ya Marsabit.
Takriban watu milioni 18 katika Pembe ya Afrika wanakabiliwa na njaa kali huku ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 40 ukiathiri eneo hilo.
Zaidi ya watu milioni nne wanaishi kaskazini mwa Kenya eneo ambalo mara nyingi husahaulika, idadi ambayo imepanda kwa kasi mwaka huu huku ukame ukikosa kushughulikiwa kwasababu ya kampeni za uchaguzi zinazoendelea.
Takriban watoto 950,000 walio chini ya miaka mitano na wanawake 134,000 wajawazito na wanaonyonyesha katika maeneo kame ya Kenya wana utapiamlo na wanahitaji msaada, kulingana na takwimu za serikali kuanzia Juni.
Njaa katika kaunti tatu zilizoathiriwa zaidi, pamoja na Marsabit, inelekea kuwa ukame mkali.
Utabiri wa Benki ya Dunia mwezi Juni kwamba ukame, pamoja na mtafaruku wa kiuchumi kutokana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, unapunguza ahueni ya Kenya kutokana na janga la coronavirus.
Hata hivyo ukame haujajitokeza sana katika ajenda ya uchaguzi huku vigogo wa kisiasa nchini Kenya wakizunguka nchi katika kempeni.
Katika mazingira magumu, kupanda kwa gharama ya maisha katika uchumi mkubwa zaidi wa Afrika Mashariki kumefunika maswala mengine.
Waandamanaji katika miji mikubwa wametishia kususia uchaguzi unaotarajiwa wa Agosti 9 ikiwa bei haitashushwa, wakiimba “hakuna chakula, hakuna uchaguzi.”
Masaibu ya kaskazini mwa Kenya kwa kiasi kikubwa hayajashughulikiwa alisema mwanauchumi Timothy Njagi kutoka Taasisi ya Sera na Maendeleo ya Kilimo ya Tegemeo jijini Nairobi.
“Niliona ni jambo la kusikitisha sana… Kwa kuzingatia kwamba huu ulikuwa mwaka wa uchaguzi, suala la ukame lingekuwa jambo muhimu la majadiliano,” aliiambia AFP.
Mvua haijanyesha kwa misimu minne mfululizo, na hali imekuwa mbaya zaidi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, imeunda hali ya ukame zaidi tangu mwanzoni mwa miaka ya 1980.
Ukame, ambao unaweza kuendelea hadi 2023 ikiwa mvua zijazo zitashindwa kama ilivyotabiriwa, pia haujapata kuzingatiwa na mataifa mengine ya nje.
Ombi la msaada kwa Ukraine limechanga dola bilioni 1.92 — karibu asilimia 86 ya lengo lake, kulingana na data ya Umoja wa Mataifa.
Ombi la msaada mdogo zaidi kukabiliana na ukame nchini Kenya imefikia asilimia 17 tu ya lengo lake.
Wakati huo huo, gharama ya kutoa misaada imepanda huku vita vya Ukraine vikifanya bei ya chakula na mafuta kupanda.
Serikali inasema imetumia zaidi ya shilingi bilioni 10 za Kenya tangu ukame huo kutangazwa kuwa janga la kitaifa mwezi Septemba.