Takriban watu 19 wameuawa katika jimbo linalokumbwa na machafuko la Sudan la Darfur, maafisa walisema Ijumaa. Katika ghasia za hivi punde zilikuwa kati ya makundi hasimu ambayo yamesababisha makumi ya watu kuuawa wiki hii.
Mapigano mapya yaliyozuka Alhamisi yameshuhudia makundi yenye silaha yakipigana katika milima ya Jebel Moon katika jimbo la Darfur Magharibi, karibu na mpaka na Chad.
Takriban âwatu 19 waliuawa na watano kujeruhiwa,â alisema Adam Regal, msemaji wa Shirika la Uratibu Mkuu wa Wakimbizi na Waliohamishwa katika Darfur, shirika huru la misaada.
Hapo awali aliripoti kuwa âwatu kadhaa walijeruhiwa na kupoteaâ na âvijiji vinne vilichomwa kabisa.â
Regal aliwashutumu wanamgambo wa Janjaweed — ambao wengi wao wamejiunga na Kikosi cha Rapid Support Forces, kinachoongozwa na Jenerali Mohamed Hamdan Daglo, naibu kiongozi wa Sudan — kwa kushiriki katika mapigano ya wiki hii âWanamgambo wamekuwa wakishambulia vijiji vya Jebel Moon. , kuchoma moto nyumba na kutumia bunduki tangu Jumapili,âkiongozi wa kabila aliiambia AFP kwa sharti la kutotajwa jina.
âHakuna vikosi vya serikali vilivyowasili tangu mashambulizi ya Alhamisi, na tunaogopa shambulio wakati wowote.â
Kati ya Jumamosi iliyopita na Jumatatu, mapigano yamesababisha vifo vya watu 16 katika eneo moja, kulingana na muungano huru wa madaktari.
Watu wengi wameuawa na mamia ya nyumba kuchomwa moto katika matukio kadhaa ya ghasia huko Jebel Moon na maeneo mengine huko Darfur katika miezi ya hivi karibuni, Umoja wa Mataifa na madaktari walisema.
Darfur iliharibiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyozuka mwaka 2003, vilivyowakutanisha waasi wa makabila madogo waliolalamikia ubaguzi ulitekelezwa na serikali ya waarabu ya rais wa wakati huo Omar al-Bashir.
Khartoum ilijibu kwa kutuma kundi la Janjaweed, hasa walioajiriwa kutoka makabila ya wafugaji wa Kiarabu, ambao walilaumiwa kwa ukatili ikiwa ni pamoja na mauaji, ubakaji, uporaji na kuchoma vijiji.
Kampeni hiyo ilikuwa ya kuteketeza nyumba na mashamba na ilisababisha vifo vya watu 300,000 na wengine milioni 2.5 kukimbia makazi yao, kulingana na UN.
Eneo hilo bado limejaa silaha na mapigano makali mara nyingi huzuka watu wanapopigania upatikanaji wa malisho au maji.
Makubaliano ya amani yalitiwa saini mwaka 2020 lakini tangu mapinduzi ya kijeshi mwezi Oktoba, Darfur imeshuhudia kuongezeka kwa ghasia, huku mamia wakiuawa katika mapigano kati ya wafugaji na wakulima.
Bashir, ambaye anatakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa tuhuma za mauaji ya halaiki huko Darfur, aliondolewa madarakani Aprili 2019 na kufungwa jela baada ya maandamano makubwa ya kupinga utawala wake wa miongo mitatu.
Mapigano ya hivi punde yanaonyesha kuvurugika kwa usalama zaidi huko Darfur kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwaka jana yaliyoongozwa na mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan ambayo yalizuia mpito kwa utawala kamili wa kiraia.
Kuongezeka kwa ghasia Darfur pia kumeshuhudia ubakaji, kuchomwa moto kwa vijiji, pamoja na kambi za Umoja wa Mataifa kuporwa.