Marais wa Afrika waliozuru Ikulu ya White House Kwa Ziara ya Kiserikali

Alhamisi tarehe 24 mei 2024, Rais wa Kenya William Ruto alifnya ziara ya kihistoria baada ya kukutana na rais wa marekani Joe Biden katika Ikulu ya White House, Washington DC Marekani. Ziara ya Ruto White House ni ya kwanza kwa zaidi ya miaka 16, tangu Rias yeyote kukutana na kufanya ziara ya kiserikali Ikulu ya White House.

Kando na Rais Ruto, Wengine waliowahi fanya ziara ya kiserikali na kukutana na rais wa marekani ni Aliyekuwa rais wa Ghana John Kufour ambaye  alifanya ziara rasmi nay a kiserikali mwaka wa 2008. Kufour alikaribishwa na Rais wakati huo George W.  Bush. Rias Bush vile vile alikuwa mwenyeji wa Aliyekuwa rais wa Kenya hayati Mwai Kibaki. Kibaki alikutana na Bush mwaka wa 2003 katika Ikulu ya White House.

Mwaka wa 1994, rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini Nelson Mandela alizuru taifa la marekani kwa ziara ya kiserikali na alilakiwa Ikulu ya White House na rais wa awamu ya 42 wa marekani, Bill Clinton.

Shehu Shagari, Rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia Nigeria mwaka wa 1979, vile vile alifanya ziara ya Kiserikali Marekani mwaka wa 1983 na kupokelewa na rais wa marekani wa awamu ya 40, Ronald Reagan.

Marais Wengine wa Afrika waliowahi zuru White House kwa safari ya Rasmi ni aliyekuwa Rais wa Tatu wa Egypt Anwar Sadat na Rais Mwanzilishi wa Tunisia Habib Bourguiba.

https://youtu.be/KxHOLXOErQA