Mashirika Kadha Kuandaa Maandamano Sambaba Na Azimio

Kiongozi wa azimio Raila Odinga ametangaza rasmi kuwa siku ya Jumatano tarehe 12/7/2023, kikosi chake kitarejea tena uwanajani. Odinga amesema maandamano yataanza na mkutano wa hadhara katika uwanja wa kihistoria ya kamkunji.

Maandanao ya azimio huenda likapigwa jeki siku ya jumatano baada ya mashirika tofauti tofauti kutangaza kujiunga na maandamano hayo.

Tayari wanaharakati wa  kijamii, chama chama madakatari na wauguzi, madereva wa magari ya uchukuzi, baadhi ya makundi ya watu wanaoishi na  walemavu, wahudumu wa Boda Boda na waendeshaji magari ya Ubar wametangaza kuandaa mgomo kushinikiza serekali  kuzingatia maslahi yao kama vile kuwapa nyongeza ya mshahara, kupunguzwa kwa gharama ya maisha na kuondoa ushuru wa mafuta.

Wanaharakati nao wanaandamana kulaani kitendo cha kuvurushwa kwa kutupiwa bomu ya kutoa machozi aliyekuwa jaji mkuu Willy Mutunga alipofika katika kituo cha polisi cha central kuwatetea waliokamatwa wakati wa maandamano.

Odinga amesema maandamano ya kesho yatafanyika kote nchini. Katika kaunti ya  Nairobi, maandamano hayo yanatarajiwa kufululu moja kwa moja hadi jiji kuu la Nairobi na amewataka wafuasi wake kujitokeza kwa wingi hata zaidi hapo kesho.

Hayo yakijiri, waziri mkuu huyo wa zamani ametangaza watukuwa wanawachukulia hatua za kisheria baadhi ya maafisa wa polisi ambao walionekana wakitumia nguvu kupindukia kwa waandamanaji hao.

Katika maandamano ya Ijuma wiki iliyopita, zaidi ya watu watano waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamanao.