Mastaa 10 wanaotaraijwa Kung’aa katika Mashindano ya AFCON 2023

Ikiwa imesalia chini ya masaa 24 kwa kindumbwendubwe cha Michuano ya ubingwa wa bara Africa AFCON, kuanza nchini ivory Coast, baadhi ya wachezaji wanaonekana kubeba matumani ya mataifa yao katika kipute hicho.

Mohamed salah ni mmoja wa wanasoka wanaotazamwa pakubwa na ulimwengu mzima kuigoza the pharaohs ya misri katika mashindano hayo. Kwa sasa Mo Salah, anayecheza soka ya kimataifa na klabu ya Liverpool, ndiye nahodha wa timu ya taifa Taifa la misri ambayo ndio wanaongoza kwa kutwa  kombe hilo kwa mara 7.

Na baada ya kuiongoza Napoli kutwaa Ubingwa wa ligi kuu ya Serie A msimuu wa 2022/23, Vitctor Osimhen ni miongoni mwa chipukizi waotazwa kuiongoza super Eagles ya Nigeria katika mashindano hayo. Osimhen mwenye umri wa miaka 25  ndiye aliyeongoza katika ufungaji wa mabao kwenye mashinda ya kufuzu AFCON 2023. Nigeria ni miongoni mwa mataifa yanayopigiwa upato kushinda mashindo hayo..Osimhen Huvalia jezi nambari tisa katika timu ya taifa ya super Eagles. Kwa sasa yeye ndiye mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa bara Africa mwaka wa 2023.

The atlas lions ya Morocco Vile vile imeorodhesha kama mataifa yanayopigiwa upato mkubwa kutwa ushindi wa makala hayo baada ya kufanya vyema katika mashindono ya kombe la dunia mwaka wa 2022. Achraf Hakimi ni mmoja wa beki waliyongaa katika timu ya morocco na anatazamiwa kuiongoza timu yake kufanya vyema.  Hakimi husakata kabumbu na miamba wa ufarasa PSG.

Sadio Mane, ambaye alifunga pingu za maisha na mpeziwake wa muda mrefu Aisha Tamba wiki mojailiyopita, anatarajiwa kuiongoza tena Teranga lions ya Senegal kuhifadhi ubingwa huo baada ya kufanya hivyo mwaka wa 2021. Mane, Nyota wa zamani wa Liverpool na Bayern munche,na kwa sasa anaitumikia klabu ya al nassir ya Saudi Arabia , ameifungia Teranga lions magoli 39 tangu alipoanza kuichezea Senegal. Senegal ni moja ya mataifa yanayopigiwa upato mkubwa kunyakua taji hilo.

Kurejea kwa Andrea Onana katika soka ya kimataifa baada ya kutangaza  kutoka kumeleta msisimko mkubwa katika timu ya taifa ya Indomitable lions ya Cameroon. Onana alikuwa ametangaza kustaafu soka ya kimataifa baada ya mzozo baina yake na shirikishola soka ya Cameroon lakini baada mzozo huo kutatuliwa mlanda lango huyo wa Manchester united aliamua kurejea tena. Licha ya kuwa na msimu panda shuka na Kalbu ya Manchester united, Onana ni mmoja wa walinda lango tajika zaidi sit u barani Africa bali ulimwengu mzima. Licha ya kwamba hatakuweko katika mchuona waowa kwanza dhidi ya na guinea, mlinda lango huyo mweye umri wa miaka 27 anatarajiwa kuwa mchumani wakati Cameroon itakuwa ikivaana na senegali .

Black stars ya Ghana vile vile itakuwa ikiwekamatumaini yake nyuma ya chipukizi namshambulizi wa west ham Mohamed Kudus. Kudus, katika msimu wake wa kwanza katika ligi ya kuu ya uingereza amewashangaza wengi kwa kuibukia kuwa nyota mahiri na Ghana inataria kutumia huduma zake kurejesha hadhi yake katika mashinda ya bara Africa.

Africa mashariki imeweka matumanini yao nyuma ya wachezaji Simon Msuva na Mbwana samatta wa taifa stars ya Tanzania. Tanzania ndio taifa peke ya Africa mashariki iliyofuzi makala hayo. Msuva na samatta kwa muda sasa wamekuwa nguzo muhimu katika ufanisi wa Taifa stars katika mashindani hayo.