Aliyekuwa waziri wa usalama wa ndani nchini Kenya Fred Matiang’i Ijumaa 24 ,2023 alidinda kufika katika ofisi za idara ya upepelezi wa jinai DCI jinsi alivyoagizwa.
Matiang’i alitakiwa kufika katika ofisi hizo kuhojiwa kuhusu madai ya maafisa wa polisi kuvamia nyumbani kwake mtaani Karen jijini Nairobi.
Matiang’i kupitia mawakili wake Danstan Omari na Sam Nyaberi amesema kuwa agizo hilo lilikuwa kinyume na sheria kwani tayari mahakama ilitoa amri ya kutokamatwa kwake.
Hii inajiri siku chache baada ya wakili wake Matiang’i Danstan Omari kutakiwa kufika pia katika ofisi za DCI kuelezea alichokijua kuhusu tukio la uvamizi nyumbani kwake Dkt Matiang’i, linalodaiwa kutekelezwa na maafisa wa polisi Februari 8 na 9 2023.
Hata hivyo Mahamaka kuu ilimwamuru mkurugenzi wa DCI Amin Mohamed akome kumtaka wakili Danstan Omari afike katika ofisi yake.
Tukio la uvamizi nyumbani kwake Mating’i lilizua hisia mseto miongoni mwa viongozi wa kisiasa na hata wakenya.