Mauaji, kupotea kwa karatasi za kupigia kura yashuhudiwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa Tanzania

Uchaguzi wa serikali za mitaa unafanyika Jumatano hii, Novemba 27 kote nchini Tanzania. Kwa jumla, zaidi ya vijiji na vitongoji 75,000 vitachagua wawakilishi wao wa mitaa kwa kipindi cha miaka mitano. Uchaguzi ambao unafanyika baada ya miezi kadhaa ya mivutano ya kisiasa nchini na kutoweka kwa wapinzani wa kisiasa, na mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wa rais.

Hata hivyo visa vya mauji madai ya wizi na kutoweka kwa vifaa vya kupigia kura vimeshudiwa.

‘’Tumepokea taarifa za viongozi wetu kuuwawa usiku wa kuamkia leo kama ifuatavyo; Katika Kata ya Mkwese ,Kitongoji Cha Stand, Jana usiku mgombea wetu wa nafasi ya Uenyekiti Kitongoji Cha Stand alivamiwa nyumbani kwake na watu waliofahamika kuwa makada wa CCM ndipo ukatokea mzozo mkubwa, Polisi walifika nyumbani kwake na kumpiga risasi ndugu George Juma Mohamed na kufariki Dunia .Usiku wa kuamkia leo Kiongozi wetu Steven Chalamila, alivamiwa nyumbani kwake usiku na kukatwakatwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake na umauti kumkuta’’ Chadema imetangaza

Katika wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza Msimamizi wa Uchaguzi  Kiomoni Kibamba amesema mapema leo baadhi ya wananchi katika mtaa wa Lwanhima kata ya Lwanhima wamekimbia na karatasi za kupigia kura hali iliyosababisha zoezi hilo kusimama kwa muda.

Akizungumza baada ya kutimiza haki yake ya kupiga kura katika kituo cha Isamilo Kasikazini A amesema kutokana na changamoto hiyo, halmashauri ilifanya utaratibu wa kuchukua karatasi zingine na kuzipeleka kwenye kituo hicho.

“Kuna changamoto kidogo, kuna baadi ya vijana walivamia kituo na kukimbianazo, lakini tayari vijana hao wameshakamatwa na watachukuliwa hatua, na kuhusu karatasi za kupigia kura tushapeleka zingine na zoezi linaendelea,” amesema Kibamba

Katika Kijiji cha Msangano, Wilaya ya Momba mkoani Songwe, hali ni vile vile. Inadaiwa kuwepo kwa kitoa cha uchaguzi ambalo hakijasajili na ina wagombea waw a chama cha CCM pekee. Hamna wagombea wowote wa upinzani.