Mawaziri 19 wapya waapishwa Kenya

Jumla ya mawaziri 19 walioteuliwa kuhudumu katika Baraza Jipya la Mawaziri wamekula kiapo cha utendakazi. Hafla ya kuwaapisha ilifanyika leo Alhamisi katika Ikulu ya Nairobi na kuongozwa na Rais William Ruto.

Justin Muturi Taking oath as the new cabinet Secretary for Public service

Kamati ya bunge kuhusu uteuzi iliwaidhinisha mawaziri hao wateule 19 huku ikikatalia mbali uteuzi wa Stella Lang’at kuwa Waziri wa Jinsia kwa misingi kwamba hakuonyesha kuwa na ufahamu wa masuala katika wizara hiyo wakati wa usaili wake.

Akizungumza wakati wa kuapishwa kwa mawaziri hao katika Ikulu, Rais Ruto aliwataka Wakenya kuwapa fursa ya kuwatumikia akisema ana imani watabadilisha hali ya nchi na kuifanya kuwa bora zaidi.

Alice Wahome taking oath of office in the ministry of Lands

Mawaziri 19 walioapishwa baada ya kuidhinishwa na bunge ni pamoja na: Prof. Kithure Kindiki (Usalama wa Taifa) Debra Barasa (Afya), Alice Wahome (Ardhi), Julius Ogamba (Elimu), Soipan Tuya (Ulinzi), Andrew Karanja (Kilimo), Aden Duale (Mazingira), Eric Muuga (Maji na Usafi), Davis Chirchir (Barabara na Uchukuzi na Margaret Ndung’u (Habari, Mwasiliano na Uchumi wa Digitali).

 

Wengine ni John Mbadi (Fedha), Salim Mvurya (Biashara), Rebecca Miano (Utalii), Opiyo Wandayi (Nishati), Kipchumba Murkomen (Michezo), Ali Hassan Joho (Madini na Uchumi wa Baharini), Alfred Mutua (Leba), Wycliffe Oparanya (Vyama vya Ushirika) na Justin Muturi (Utumishi wa Umma).