Mchezaji kandanda atozwa faini na kupoteza udhamini kwa kumpiga teke paka wake

Mshambulizi wa West Ham United Kurt Zouma

Mchezaji wa klabu ya West Ham Kurt Zouma ameadhibiwa na klabu yake na kupoteza mkataba wa udhamini na kampuni ya Adidas baada ya video inayomuonyesha akimpiga teke paka wake kusambaa mitandaoni. Vitality, kampuni ya Bima ambayo pia ni miongoni mwa wafadhili wakuu wa West Ham, pia ilisitisha ushirikiano wake na klabu hiyo “mara moja.”

Mchezaji mwenzake wa West Ham Michail Antonio amesema kuwa ubaguzi wa rangi katika michezo na jamii unabaki kuwa suala kubwa zaidi linalohitaji kushughulikiwa kuliko hilo la Zouma kumpiga paka wake.

Beki wa kimataifa wa Ufaransa Zouma mwenye umri wa maika 27, amezua taharuki kati ya watu kutokana na kitendo chake kilichofichuliwa kwenye mitandao ya kijamii. Shirika la kutetea haki za wanyama la RSPCA baadaye liliwachukua paka wake na kuwapeleka katika hifadhi yao.Kumekuwa na mwito wa kuvunjwa kwa mkataba wake.

Mshambulizi wa West Ham United Kurt Zouma

Suala hilo bado halijafikia hatua hiyo, ingawa vikwazo zaidi vinaweza kufuata, na Antonio anaamini hatua kama hiyo inastahili kuchukuliwa dhidi ya wale wanaohusika katika vitendo vya ubaguzi wa rangi.

Zouma alipata shutuma nyingi kwa kitendo chake, huku klabu yake ikimpiga faini ya mshahara wa wiki mbili wa jumla ya euro 250,000.

Mchezaji huyo aliomba msamaha akisema ilikuwa kesi ya pekee ambayo haitatokea tena lakini uharibifu ulikuwa umefanywa.

“Nataka kuomba msamaha kwa matendo yangu. Pia naomaba msamaha sana kwa mtu yeyote ambaye alichukizwa na video hiyo. Ningependa kuwahakikishia kuwa paka hao wako sawa na wana afya njema. Wanapendwa na kuthaminiwa na familia yetu yote, na tabia hii ilikuwa tukio la kipekee ambalo halitatokea tena,” alisema Zouma.

Tukio la Zouma kuadhibiwa limeibua mjadala mzito #BlackLivesMatter kwenye mitandao ya kijamii na wengine kuhoji adhabu aliyopewa.

Mshambulizi wa West Ham Michail Antonio alisema alipoulizwa kuhusu Zouma: “Nina swali kwako – unafikiri alichokifanya ni kibaya zaidi kuliko ubaguzi wa rangi?

“Sikubaliani na jambo ambalo amefanya”.Sikubaliani na alichofanya hata kidogo,Lakini kuna watu ambao wamehukumiwa na kukamatwa kwa ubaguzi wa rangi na wamecheza mpira baadaye.

“Ninapaswa kuuliza swali hili kwa kila mtu sasa – je, kile amefanya kibaya zaidi kuliko kile ambacho watu wamefanya ambao wamehukumiwa kwa ubaguzi wa rangi?”

Kando na kuhusika katika kashfa hiyo, Zouma alishirikishwa katika mchezo wa ligi ya Premier dhidi ya timu ya Watford siku ya Jumanne.

Meneja wa West Ham David Moyes yuko njia panda kuhusu timu yake kucheza dhidi ya Leicester Jumapili, huku kukiwa na shinikizo kali kumuacha nje beki Kurt Zouma.

Lakini uamuzi wa Moyes kumchezesha Zouma katika ushindi wa 1-0 Jumanne dhidi ya Watford, saa chache baada ya video kuibuka ya Mfaransa huyo akimpiga teke paka wake, ulionekana na wengi kama uamuzi mbaya.

Uamuzi wa Moyes kumchezesha Zouma Jumanne umekosolewa vikali na watu mashuhuri katika michezo na siasa.

Zaidi ya watu 300,000 wametia saini ombi la mtandaoni la kumtaka Zouma ashtakiwe.

https://youtu.be/UCl5_q1x0Kk