Meli yenye bendera ya Tanzania imezama kusini mwa Kisiwa cha Kish nchini Iran

Meli yenye bendera ya Tanzania imeripotiwa  kumezama kusini mwa Kisiwa cha Kish nchini Iran, shirika la habari la Iran la Tasnim liliripoti Jumatano, na kuongeza kuwa sababu ya tukio hilo ilikuwa ikichunguzwa.

Shirika hilo lilimnukuu afisa mmoja wa Iran akisema wafanyakazi hao tisa waliokolewa kutoka kwa meli hiyo, iliyokuwa imebeba tani 2,500 za saruji nyeupe.

 

Tukio hilo lilitokea mwendo wa saa 13:30 kwa saa za huko siku ya jumatano. Meli hiyo ilikuwa ikitoka Ras Al Khaimah katika Umoja wa Falme za Kiarabu kuelekea Bandari ya Shuaiba nchini Kuwait ilipoanza kuzama maji takriban maili mbili kusini mwa Kisiwa cha Kish, na kusababisha tangazo la dharura.