Mfalme Charles wa tatu wa Uingereza ameelezea majuto, huzuni na masikitiko mkubwa kutokana na dhuluma zilizotekelezwa na serikali ya Uingereza dhidi ya wakenya wakati wa harakati za kupigania uhuru wa taifa la Kenya.
Mfalme, akiandamana na malkia Camilla, alisema hayo wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais William Ruto na Mama Rachel Ruto Jumanne jioni katika ikulu ya Nairobi, Kenya
Rais Ruto alimualika mfalme Charles na malkia wake kuzuru maeneo kadha katika taifa hilo la afrika mashariki yenye mandhari ya kuvutia na kupendeza jijini Nairobi
Wakati wa dhifa hiyo iliyohudhuriwa na kinara wa upinzani Raila Odinga, mfalme Charles alielezea ari yake ya kukutana na waathiriwa wa dhuluma hizo za kihistoria.
Alikariri umuhimu wa pande zote mbili kushughulikia dhuluma hizo za kihistoria kwa njia iliyowazi.
“Ni muhimu sana kwangu kukutana na baadhi ya wale maisha yao na jamii zao ziliathiriwa pakubwa na dhuluma hizo,” alisema Mfalme Charles.
Ziara hiyo ya kifalme hapa nchini, itaangazia jinsi Kenya na Uingereza zitashirikiana pamoja katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa fursa za ajira kwa vijana.
Mfalme Charles Mapema Jumatano alizuru makaburi ya Kariokor, Jijini nairobi ambapo alitoa heshima zake wa wafu. Makaburi ya kariokor ni ya kihistoria kwani baadhi ya watu waliopigana katika vita vya pili vya dunia walizikwa.
Siku ya Alhamisi, Mfalme Charles atakuwa akizuru pwani ya kenya