klabu ya Simba imefuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kulabua Horoya ya Guinea magoli 7-0 katika mchezoo wa kufana uliopigwa kwenye Uga wa kimataifa wa Benjamin Mkapa.
Shujaa katika mchezo huo alikuwa Clatous Chama aliyefunga Hat-Trick dakika ya 10, 36 na 70 huku Jean Baleke akifunga mawili dakika ya 32, 65 na Sadio Kanoute akifunga pia mawili dakika ya 55 na 87.
Ushindi huu ni wa kwanza na mkubwa sana kwa wekundu wa msimbazi katika hatua ya makundi baada ya kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya Vipers SC kwenye michezo miwili iliyopita iliyopigwa jijini Kampala na Dar es Salaam.
Vile Vile Chama anakuwa ni mchezaji wa kwanza wa miamba wa soka Tanzania katika hatua hii ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kufunga mabao matatu.
Hii inajiri tu siku chache tu tangu nyota huyo achaguliwe na shirikisho la soka barani Africa CAF kuwa mchezaji bora wa wiki.
Kutokana na ushindi huo, simba wamepokezwa Milion 35 pesa taslimu ya Tanzania baada ya rais Samia Suluhu kuwahidi millioni tano kwa kila bao