Search
Close this search box.
Europe

Michezo ya Jumuiya ya Madola kuzinduliwa kwa mbwembwe mjini Birmingham

30

Zaidi ya wanariadha 5,000 watapata nafasi ya kushiriki katika michezo ya Jumuiya ya Madola katika jiji la Birmingham nchini Uingereza kuanzia Ijumaa.

Washindani kutoka mataifa na maeneo 72 – ambayo mengi yao ni makoloni ya zamani ya Uingereza – watakuwa wakiwania medali katika michezo 19 kwa siku 11.

Mbali na mashindano ya riadha na matukio ya kuogelea, kriketi ya wanawake ya Twenty20 itashirikishwa kwa mara ya kwanza na mpira wa vikapu wa 3×3 utaangaziwa kwa mara ya kwanza.

Kuna program ya michezo kwa walemavu iliyojumuishwa katika hafla zingine.

Michezo hiyo, inayofanyika kila baada ya miaka minne, mara nyingi hukosolewa kama masalio ya kimichezo lakini mwaka huu michezo hiyo itazinduliwa kwa mtindo katika sherehe za ufunguzi siku ya Alhamisi, zikiongozwa na bendi ya pop ya miaka ya 1980 Duran Duran, iliyoanzishwa Birmingham.

Mabingwa wa michezo Australia wameongoza jedwali la medali katika kila Michezo tangu 1990 isipokuwa mwaka wa 2014, wakati Uingereza ilimaliza kileleni katika mashindano yaliyofanyika mjini Glasgow – mara ya mwisho mashindano hayo yalifanyika katika ardhi ya Uingereza.

Uingereza, Uskoti, Wales na Ireland Kaskazini hushindana kama timu tofauti wakati wa michezo ya Jumuiya ya Madola badala ya nchi moja Uingereza.

Comments are closed

Related Posts