Mohamed Salah aling’ara wakati Misri ilipofuzu kushiriki nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika siku ya Jumapili. Misri ilijiunga na Senegal katika hatua ya nne bora katika mechi iliyochezwa uwanjani Olembe mjini Yaounde ambako watu wanane walifariki dunia baada ya msukumano wiki moja iliyopita.
Shirikisho la Soka Afrika lilisema kuwa nusu fainali ya pili tarehe Februari 3 kati ya wenyeji na Misri na fainali Februari 6 itafanyika katika uwanja wa Olembe baada ya kuondoa zuio la kuchezwa kwenye uwanja huo ambapo watu wanane walifariki akiwemo mtoto mchanga mnamo Januari 24.
“Baada ya kuzingatia mapendekezo na ahadi kutoka kwa serikali kuhusu kuboresha usalama…Kamati ya Maandalizi ya CAF ilikubali kwa kauli moja kuondoa vizuizi viliyowekewa Uwanja wa Olembe,” bodi inayosimamia soka ya Afrika ilisema katika taarifa yake.
Maafa hayo yalitokea kabla ya mechi ya Jumatatu iliyopita ya hatua ya 16 bora kati ya wenyeji Cameroon na Comoro, wakati mashabili waliposongamana kwenye lango la kusini mwa uwanja.
Watu 38 pia walijeruhiwa kweney msongamano huo. Mshuhuda wameliambia shirika la habari la AFP kwamba umati wa watu walisukumana mlangoni kabla polisi kuufungua.
Waziri wa michezo wa Cameroon siku ya Ijumaa alilaumu “uamuzi mbaya” wa vikosi vya usalama kufungua lango hilo lililosababisha maafa, na akatangaza hatua zitakazochukuliwa kuhakikisha kuwa Uwanja wa Olembe unaweza kufunguliwa tena.
Uwanja wa Olembe una viti 60,000 uliojengwa mahsusi kwa ajili ya michuano hiyo, ulipokonywa nafasi kwa michuano ya robo fainali iliyopaswa kuchezwa hapo, na mechi hiyo badala yake ikahamishiwa kwenye uwanja wa Ahmadou Ahidjo pia mjini Yaounde.
Hiyo ilimaanisha kuwa mechi mbili zilichezwa katika uwanja wa Yaounde siku ya Jumapili, huku Misri ikitoka nyuma na kuishinda Morocco 2-1 katika muda wa nyongeza kabla ya Senegal kuifunga Equatorial Guinea 3-1.
– Misri yaichabanga Morocco
Morocco walikuwa uongozini baada ya mkwaju wa penalti kutoka kwake Sofiane Boufal uliomfanya nahodha wa Misri, Salah kusawazisha mapema katika kipindi cha pili.
Misri mabingwa bara mara saba walipata bao la ushindi katika dakika ya 100.
Mane aifungia Senegal
Alipokuwa akitoka uwanjani, Salah aligongana na mchezaji mwenzake wa Liverpool Sadio Mane akiwasili kwa mechi ya Senegal. Famara Diedhiou aliifungia Senegal bao la kwanza kabla Jannick Buyla kusawazisha katika kipindi cha pili.
Hata hivyo, Cheikhou Kouyate na Ismaila Sarr waliifungia Senegal katika nusu fainali na watakutana na Burkina Faso siku ya Jumatano kwenye Uwanja huo huo wa Ahmadou Ahidjo katika mji mkuu wa Cameroon.
Burkina Faso ilishinda Tunisia 1-0 siku ya Jumamosi na kutoa ahueni kwa nchi iliyotikiswa na kuondolewa madarakani kwa Rais Roch Marc Christian Kabore wiki iliyopita katika mapinduzi ya kijeshi.
Wenyeji Cameroon waliishinda Gambia 2-0 katika robo fainali mjini Douala katika mechi yao ya kwanza uwanjani Olembe, na sasa watarejea huko kumenyana na Misri siku ya Alhamisi katika mkutano wa timu hizo mbili zilizo na mataji mengi zaidi ya Kombe la Mataifa.