Wanawake wawili, mmoja raia wa Austria na mwingine raia wa Romania, waliuawa katika shambulio la papa wiki hii kwenye pwani ya Misri, wizara ya mazingira ya Misri na wizara za mambo ya nje za watalii hao zilisema Jumapili.
“Wanawake wawili walishambuliwa na papa walipokuwa wakiogelea” katika eneo la Sahl Hasheesh kusini mwa Hurghada kwenye Red Sea, wizara ya Misri ilisema Jumapili kwenye Facebook, ikiripoti kwamba wote wawili walikufa.
Shirika la habari la Austria APA lilisema mmoja wa wanawake hao alikuwa na umri wa miaka 68 ambaye alikuwa likizoni nchini Misri.
Wizara ya mambo ya nje ya Austria ilithibitisha kwa AFP Jumapili ‘kifo cha raia wa Austria nchini Misri,’ bila kutoa maelezo zaidi.
Ikinukuu taarifa zilizopokelewa kutoka kwa mamlaka za Misri, wizara ya mambo ya nje ya Romania ilithibitisha kuwa siku ya Jumapili ‘kifo cha raia wa Romania’ ambacho ‘kilionekana’ kilisababishwa na ‘shambulio la papa’ karibu na Hurghada.
Gavana wa eneo la Red Sea Amr Hanafi siku ya Ijumaa aliamuru kufungwa kwa fuo zote katika eneo hilo kwa siku tatu baada ya ‘mtalii wa Austria kung’olewa mkono wake wa kushoto katika shambulio la papa.”
Watumiaji wa mitandao ya kijamii siku ya Ijumaa walionyesha video ikimuonyesha muogeleaji akihangaika kabla ya kile kilichoonekana kuwa damu nyingi kutokea karibu naye.
Kikosi kazi kinafanya kazi ‘kutambua sababu za kisayansi na mazingira ya shambulio hilo’ na kubaini ‘sababu za tabia ya papa iliyosababisha tukio hilo,’ wizara ya mazingira ilisema Jumapili.
Red Sea ni kivutio maarufu cha watalii, ambapo papa ni wa kawaida lakini si sana wao kuwawashambulia watu wanaoogelea ndani ya mipaka iliyoidhinishwa.
Mnamo 2018, mtalii wa Czech aliuawa na papa kwenye ufuo wa Red Sea.
Shambulio kama hilo lilimuua mtalii wa Ujerumani mwaka 2015. Mnamo 2010, mfululizo wa mashambulizi matano ndani ya siku tano karibu na ufuo wa kivutio cha watalii Sharm el-Sheikh kilimuua Mjerumani mmoja na kuwajeruhi watalii wengine wanne wa kigeni.
Misri kwa sasa inajitahidi kukabiliana na mfumuko wa bei unaoongezeka na kudorora kwa thamani ya sarafu.
Nchi hiyo inategemea sana mapato ya utalii kutoka Red Sea, ambayo inachangia asilimia 65 ya watalii wanaozuru nchini.
Sekta ya utalii imekumbwa na mapigo mfululizo katika muongo mmoja uliopita, ikiwa ni pamoja na ghasia za mwaka 2011, machafuko yaliyofuata na janga la coronavirus.