Mke Wa Mhubiri Tata Paul Mackenzie Akamatwa Kilifi

Polisi Jumatatu walimkamata mke wa kasisi tata Paul Mackenzie katika uchunguzi unaoendelea kuhusu dhehebu na imani potovu ukanda wa pwani wa kenya.

Rhoda Mumbua Maweu alikamatwa kutoka kwa nyumba yake huko Mtwapa pamoja na shangazi yake Jumatatu usiku, polisi walisema.

Kikosi cha uchunguzi kilisema kuwa yeye ni mtu wa Mumbua ni baadhi ya washukiwa wa kuu katika kesi ambayo zaidi ya watu 110 wamefariki na kuzikwa msitu wa shakahola baada ya kufunga hadi kufa

Polisi walisema Mumbua ametambuliwa kama mhusika mkuu katika shughuli za kanisa hivyo hatua ya kumkamata.

Mackenzie ameshutumiwa kwa kuwahadaa watu kupitia mafundisho potovu, yaliyokithiri ya kidini na hofu ya wasiojulikana katika kutafuta wokovu, na kusababisha vifo vya watu wengi.

Kwa sasa MackenzieYuko chini ya ulinzi wa polisi kwa madai ya kuhubiri fundisho linalowahimiza wafuasi wake kujiua kwa njaa ili kufika mbinguni haraka.

Waathiriwa wengine wanasemekana kunyongwa.

Polisi wamekuwa wakikagua rekodi za simu za Mackenzie na kuwahoji watu waliounganishwa na kanisa hilo.

Ilikuwa wakati wa mchakato huu ambapo jina la Mumbua liliibuka kama mmhusika mkuu

Mumbua alaitambulika kuwa yeye  ndiye ‘meneja wa rasilimali watu’ kwa utawala wa Mackenzie.

Hadi sasa miili 110 imetolewa na operesheni inaendelea katika msitu wa Shakahola kwa kutumia teknolojia na uchunguzi wa anga.