Mkewe Hakimi Apigwa Na Butwaa Baada Ya Kugundua Nyota Huyo ‘Hamiliki’ Chochote

Nyota  wa kimataifa wa Morocco Achraf Hakimi amezua gumzo kali ulimwengu mzima baada ya mke wake kugundua kuwa ''hamiliki' chochote licha ya kupata mamilioni  ya Euro akiwa na Klabu Paris Saint Germain ya Ufaransa na timu ya taifa ya soka ya Morocco.

Ugunduzi huu ulifanywa wakati wa kesi za talaka zinazoendelea mahakamani baada ya mkewe, Hiba Abouk, kuwasilisha talaka na kuomba nusu ya mali na pesa zote alizomiliki mwanasoka huyo.

Na kwa mshangao, aligundua kuwa Hakimi, mwenye 24, alikuwa amesajili mali na pesa zake zote kwa jina la mama yake, na kila alipohitaji chochote, alikuwa akimwomba mama yake amnunulie.

Nyumba zake zote, magari, nguo, na vito vyake vyote vilipatikana kuwa katika jina la mama yake, na mamilioni ya mishahara yake yaliwekwa kwenye akaunti zenye jina la mama yake.

Iliripotiwa kuwa asilimia 80 ya vitu vyote alivyo navyo vimesajiliwa kwa jina la mamake.

Wanandoa hao walianza kuchumbiana mnamo 2018 na walioana mnamo 2020 na wana watoto wawili wa kiume. 
Abouk aliwasilisha talaka mnamo Machi 2023.

 Hakimi anayechunguzwa huko Paris, Ufaransa, kwa madai ya ubakaji amekuwa na matazo na ndoa yake na mwigizaji na mwanamitido huyo raia wa uhispania.

Hatua ya Hakimi kutosajili utajiri wake kwa jina lake limezua mdahalo mkali duniani haswa katika mitandao ya kijamii.
Wengi wameacha vinywa wazi na mshangao wasijue lakusema. Lakini wengine  wamemsifu kwa kuwa ‘mwenye hekima’ na gwiji wa kulinda mali zake; huku wengine wakimtukana Hakimi na mama yake.