Rais wa Senegal Macky Sall siku ya Jumapili alisema atasafiri hadi Urusi na Ukraine hivi karibuni kwa niaba ya Umoja wa Afrika,kama rais wa muungano huo.
Safari hiyo ilikuwa ifanyike Mei 18 lakini haikufanyika kutokana na masuala ya ratiba na tarehe mpya kupendekezwa, Sall alisema katika mkutano na waandishi wa habari na Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani anayezuru nchini humo.
Alikuwa amepokea ruksa kutoka kwa Umoja wa Afrika kuchukua safari hiyo, ambayo Urusi ilikuwa imetoa mwaliko, aliongeza.
“Mara tu tarehe mpya itakapowekwa, bila shaka nitaenda Moscow na pia Kyiv,” Sall alisema.
“Pia tumekubali kuwakutanisha wakuu wote wa nchi za Umoja wa Afrika wanaotaka kukutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ambaye ameeleza haja ya kuwasiliana na wakuu wa nchi za Afrika.”
“Hilo pia litafanyika katika wiki zijazo.”
Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, ambao umeathiri vibaya uchumi wa Afrika kutokana na kupanda kwa bei ya nafaka na uhaba wa mafuta, umepokelewa tofauti na mataifa Afrika yaliyogawanyika.
Mapema mwezi Machi, Senegal ilijizuia kupigia kura azimio la Umoja wa Mataifa — lililopitishwa kwa wingi — ambalo liliitaka Urusi kujiondoa Ukraine.
Hata hivyo, wiki chache baadaye muungano huo ulipiga kura kuunga mkono azimio jingine la kutaka Urusi isitishe vita.
Takriban nusu ya mataifa ya Afrika yalijizuia au hayakupiga kura katika kura mbili za maazimio.
Sall pia alisema Senegal itakuwa tayari kusambaza gesi asilia ya LNG kuenda Ulaya wakati bara hilo likijaribu kujiondoa kwenye vyanzo vya nishati vya Urusi.
Pamoja na nchi jirani ya Mauritania, Senegal inatarajia kutafuta amana za gesi na mafuta zinazopatikana katika bahari ya Atlantiki katika miaka ya hivi karibuni.
Sall amekadiria uzalishaji wa LNG kuanzia Desemba 2023 na kufikia tani milioni 10 kwa mwaka katika mwaka wa 2030. Kiongozi huyo wa Senegal alisema aliiomba Ujerumani kuisaidia Senegal kuendeleza miradi ya siku zijazo.
Scholz alisema majadiliano yanapaswa kuendelea “kwa kina” kwa sababu ni kwa manufaa yetu kufikia maendeleo”