Mamlaka za Marekani zimethibitisha kukamatwa kwa Tyler Robinson, kijana wa miaka 22, kwa tuhuma za kumuua mwanaharakati mashuhuri wa mrengo wa kulia Charlie Kirk.

Tyler Robinson alikamatwa baada ya jamaa wa familia kumfikisha kwa polisi, hatua iliyohitimisha msako wa saa 33 uliofuatia tukio hilo la kushtua.
Kirk, mwenye umri wa miaka 31, aliuawa kwa risasi moja ya shingoni akiwa anahutubia hadhira kubwa katika Chuo Kikuu cha Utah Valley mnamo Septemba 10.
Gavana wa Utah Spencer Cox alitangaza kukamatwa kwa mshukiwa akisema, “We got him,” na kufichua kuwa risasi zilizotumika zilikuwa na maandishi ya kupinga ufashisti, ikiwemo ujumbe uliosema “Hey, fascist! Catch!”.
Rais Donald Trump aliamuru bendera zipeperushwe nusu mlingoti na kutangaza kuhudhuria mazishi ya Kirk, ambaye alikuwa mshirika wake wa karibu katika kampeni za vijana.
Trump pia alieleza kuwa anataka adhabu ya kifo kwa mshukiwa. Mwili wa Kirk ulisafirishwa hadi Phoenix kwa ndege rasmi ya Makamu wa Rais JD Vance, aliyeonekana akiandamana na jeneza hadi Air Force Two.
Cherlie Kirk ni nani?
Charlie Kirk alikuwa mmoja wa sauti zenye ushawishi mkubwa katika siasa za mrengo wa kulia nchini Marekani. Alizaliwa mwaka 1993 na kufariki kwa kupigwa risasi mnamo Septemba 10, 2025, akiwa na umri wa miaka 31.
Umaarufu wake ulijengwa juu ya uwezo wake wa kuwasiliana moja kwa moja na vijana, hasa kupitia mitandao ya kijamii na mijadala ya wazi vyuoni.
Mnamo mwaka 2012, akiwa na umri wa miaka 18 tu, Kirk alianzisha shirika la ‘Turning Point USA’, ambalo lililenga kueneza maadili ya kihafidhina miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vikuu. Kupitia shirika hilo, alijijengea jina kama mtetezi wa uhuru wa kujieleza, umiliki wa bunduki, na sera kali za uhamiaji.
Alijulikana kwa kauli zake kali kuhusu masuala ya jinsia, dini, na utambulisho wa taifa—mitazamo iliyomfanya kuwa mtu wa mvutano mkubwa katika siasa za Marekani.
Kirk alikuwa na uwezo wa kipekee wa kuvutia hadhira ya vijana kupitia majukwaa kama TikTok, Instagram, na YouTube. Alitumia video fupi za mijadala yake vyuoni kueneza ujumbe wake, mara nyingi akionyesha jinsi alivyowakabili wapinzani wake kwa hoja kali na ucheshi wa kisiasa.
Umaarufu wake ulizidi kuimarika alipokuwa mshirika wa karibu wa Rais Donald Trump, akisaidia kuvutia kura za vijana katika uchaguzi wa mwaka 2024.
Ingawa alikosolewa vikali na wapinzani wake kwa kauli zinazodaiwa kuwa za chuki au ubaguzi, hata wakosoaji wake walikiri kuwa Kirk alikuwa tayari kujibizana hadharani na kutoa nafasi kwa mijadala ya wazi. Alionekana.