Shirika la UNICEF, limeripoti kuongezeka kwa visa vya ubakaji miongoni mwa watoto wadogo katika taifa la Sudan ambapo vita vya wenyewe kwa wenyewe bado vinashuhudiwa.

Kulingana na ripoti ya hivi karibuni, wanaume wenye silaha wamekuwa wakibaka na kuwadhulumu watoto wadogo, ya hivi punde ikiwa ni mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja.
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa ukatili wa kingono umetumika sana kama silaha ya vita katika mgogoro wa karibu miaka miwili.
UNICEF imebaini kuwa kesi 221 za ubakaji dhidi ya watoto zimeripotiwa rasmi tangu mwanzo wa mwaka 2024, lakini idadi halisi inaweza kuwa kubwa zaidi. Waathiriwa ni pamoja na wavulana na wasichana, ambapo theluthi moja ya waathiriwa ni wavulana.
Ripoti hiyo pia inaelezea uzoefu wa kutisha wa manusura, ikiwa ni pamoja na watoto wadogo ambao wamepitia unyanyasaji usioweza kufikirika.
Matumizi ya ukatili wa kingono kama mbinu ya vita ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na yana madhara makubwa kwa waathiriwa na familia zao